عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَا يَنْظُرُ اللهُ إِلَى رَجُلٍ أَتَى رَجُلًا أَوِ امْرَأَةً فِي دُبُرٍ».
[صحيح] - [رواه الترمذي والنسائي في الكبرى] - [السنن الكبرى للنسائي: 8952]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hamtazami Mwenyezi Mungu mtu ambaye kamuingilia mwanaume au mwanamke katika tupu yake ya nyuma".
[Sahihi] - - [السنن الكبرى للنسائي - 8952]
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ahadi kali ya adhabu kuwa Mwenyezi Mungu hatomtazama mtazamo wa huruma mwanaume aliyemuingilia mwanaume mwenzake katika utupu wake wa nyuma, au mwanamke katika utupu wake wa nyuma, nakuwa hilo ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa.