عَن أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«لَا يَنْظُرُ الرَّجُلُ إِلَى عَوْرَةِ الرَّجُلِ، وَلَا الْمَرْأَةُ إِلَى عَوْرَةِ الْمَرْأَةِ، وَلَا يُفْضِي الرَّجُلُ إِلَى الرَّجُلِ فِي ثَوْبٍ وَاحِدٍ، وَلَا تُفْضِي الْمَرْأَةُ إِلَى الْمَرْأَةِ فِي الثَّوْبِ الْوَاحِدِ».

[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Asiangalie mwanaume katika uchi wa mwanaume mwenzie, wala mwanamke kutazama uchi wa mwanamke mwenzie, na wala asijifunike mwanaume na mwanaume mwenzie shuka moja, na wala mwanamke asijifunike na mwanamke mwenzie shuka moja".

Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanaume kutazama uchi wa mwanaume mwenzie, au mwanamke kutazama uchi wa mwanamke mwenzie.
Uchi: Ni kila kinachoonewa aibu kinapodhihiri, na uchi wa mwanaume ni kati ya kitovu chake na magoti yake, Na mwanamke mwili wake wote ni uchi kwa mwanamke asiye mume wake au ndugu wa damu, na upande wa wanawake kwa ndugu zao wa damu, anaweza kuonyesha viungo ambavyo kwa desturi ya kawaida huonekana wakati wa kufanya kazi zake za nyumbani.
Na amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kukaa faragha mwanaume na mwanaume mwenzake ndani ya nguo moja, au ndani ya kifuniko kimoja wakiwa uchi, na mwanamke kukaa faragha na mwanamke mwenzie ndani ya nguo moja au ndani ya kifuniko kimoja wakiwa uchi; kwa sababu kitendo hicho huenda kikapelekea kila mmoja kugusa uchi wa mwenzie, na kuugusa ni haramu ni kama kuuangalia, bali hilo ni haramu zaidi; kwa sababu linapelekea katika uovu mkubwa.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Katazo la kutazama uchi, isipokuwa mume na mke wake.
  2. Hima ya Uislamu juu kuisafisha jamii, na kufunga njia zinazopelekea katika machafu.
  3. Inaruhusiwa kuangalia uchi kukiwa na haja ya kufanya hivyo, kama matibabu na mfano wake, na isiwe kwa matamanio.
  4. Muislamu ameamrishwa kusitiri uchi wake na kuinamisha macho yake kutotazama uchi wa mwenzie.
  5. Kumetajwa pekee wanaume kuwatazama wanaume wenzao na wanawake kuwatazama wanawake wenzao; kwa sababu ndio kishawishi kikubwa katika kutazama na kufunua uchi.