+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«صِنْفَانِ مِنْ أَهْلِ النَّارِ لَمْ أَرَهُمَا، قَوْمٌ مَعَهُمْ سِيَاطٌ كَأَذْنَابِ الْبَقَرِ يَضْرِبُونَ بِهَا النَّاسَ، وَنِسَاءٌ كَاسِيَاتٌ عَارِيَاتٌ مُمِيلَاتٌ مَائِلَاتٌ، رُؤُوسُهُنَّ كَأَسْنِمَةِ الْبُخْتِ الْمَائِلَةِ، لَا يَدْخُلْنَ الْجَنَّةَ، وَلَا يَجِدْنَ رِيحَهَا، وَإِنَّ رِيحَهَا لَيُوجَدُ مِنْ مَسِيرَةِ كَذَا وَكَذَا».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2128]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Aina mbili za watu ni miongoni mwa watu wa motoni, sijawaona (katika zama zake Mtume), watu walio na mijeledi mithili ya mikia ya Ng'ombe wakiwapiga watu, na wanawake waliovaa na wako uchi, wanenguaji wakatikaji, vichwa vyao ni kama nundu za Ngamia zenye kuyumba (huku na kule), hawa, hawatoingia peponi, na wala hawatoipata harufu yake, na hakika harufu yake hupatikana umbali wa masafa kadhaa wa kadhaa".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2128]

Ufafanuzi

Anatahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu aina mbili za watu ambao ni katika watu wa motoni, hajawaona na hawakuwepo katika zama zake, bali aina hizo zitatokea baada yake:
Aina ya kwanza: Ni watu walio na Mijeledi mirefu kama mikia ya Ng'ombe, wakiwapiga watu kwayo, nao ni Polisi na wasaidizi wa viongozi wasiowaadilifu, wanaowapiga watu bila hatia.
Aina ya pili: Ni wanawake waliovua vazi la heshima na haya walizoumbiwa nazo mwanamke kawaida.
Na sifa zao: Kwa muonekano wamevaa, na kwa uhalisia wako uchi; kwa sababu wamevaa nguo nyepesi zinazoonyesha ngozi, na wamefunika sehemu ndogo tu katika mili yao na wameacha wazi sehemu nyingine; kwa ajili ya kuonyesha urembo wao, nyoyo za wanaume zinavutika kwao kwa sababu ya mavazi yao, na kutembea kwao kwa maringo, wakinengua mabega yao, na wanawavutia wanawake wengine pia katika kupinda kimaadili, na kupotea waliko tumbukia ndani yake, Na miongoni mwa sifa zao pia: Vichwa vyao ni mfano wa nundu za Ngamia zilizopinda, utawakuta wakiipa kipaumbele mionekano ya vichwa vyao, wakiikuza kwa kukunja misuko na mfano wake, Na kufananishwa na nundu za Ngamia, ni kwa sababu kuinuka kwa nywele zao na misuko yao juu ya vichwa vyao, na kuzikunja kwao kwa sababu ya misuko mpaka zinalalia upande mmoja wa kichwa kama inavyolalia upande mmoja nundu ya Ngamia. Mwanamke atakayekuwa na sifa hizi, atakuwa na ahadi hii kali ya kutoingia peponi na wala hatopata harufu yake na wala hatoikaribia, na harufu ya pepo hupatikana na hunuswa kutoka masafa ya mbali.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية التشيكية Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Uharamu wa kuwapiga watu na kuwaudhi bila dhambi yoyote waliyoifanya au dhambi walilolichuma.
  2. Ni haramu kuwasaidia watenda dhulma katika dhulma yao.
  3. Ni haramu wanawake kutoka bila haja ya msingi na kujiachia katika mavazi, na kuvaa nguo za kubana zenye kuonyesha, zinazoonyesha uchi au kuuchora.
  4. Kumhimiza mwanamke wa kiislamu juu ya kushikamana na amri za Mwenyezi Mungu, na kujiweka mbali na yale yenye kumkasirisha, na kumfanya astahiki kupata adhabu chungu na ya kudumu Akhera.
  5. Hadithi hii ni dalili ya utume wake rehema na amani ziwe juu yake, kiasi kwamba ametoa habari rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mambo ya ghaibu ambayo hayajatokea, na yametokea kama alivyoeleza.