+ -

عَنْ جَرِيرِ بْنِ عَبْدِ اللهِ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ:
سَأَلْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ نَظَرِ الْفُجَاءَةِ فَأَمَرَنِي أَنْ أَصْرِفَ بَصَرِي.

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2159]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Jariri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Nilimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu kutazama ghafla, akaniamrisha nigeuze jicho langu.

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2159]

Ufafanuzi

Jariri bin Abdullah Mwenyezi Mungu amuwie radhi, alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mwanaume kumwangalia mwanamke wa kando ghafla bila kukusudia? Basi akamuamrisha rehema na amani ziwe juu yake kuwa aelekeze uso wake pembeni upande wa pili mara anapojua hilo, na hatokuwa na dhambi juu yake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kimalayo Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo la kuinamisha macho.
  2. Tahadhari ya kutazama kwa muda katika yale yaliyoharamishwa kuyatazama jicho linapodondokea ghafla na pasina kukusudia.
  3. Ndani ya hadithi kuna uharamu kwa kuwatazama wanawake, jambo ambalo waliishi nalo Maswahaba, kwa ushahidi wa kuwa Jariri radhi za Allah ziwe juu yake alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa endapo litaangukia jicho lake katika kumtazama mwanamke pasina kukusudia, je hukumu yake itakuwa sawa na aliyekusudia kutazama?.
  4. Na pia inaonyesha namna sheria ilivyotilia maanani masilahi ya waja, kwa kuwaharamishia kuwatazama wanawake, kwakuwa swala hilo linaambatana na maovu ya dunia na Akhera.
  5. Kurejea Maswahaba kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kumuuliza katika yale yanayowatatiza, na hivi ndivyo inavyotakiwa kwa watu wote kurejea kwa wanachuoni wao na kuwauliza katika yale yanayowatatiza.