عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:
«حُجِبَتِ النَّارُ بِالشَّهَوَاتِ، وَحُجِبَتِ الْجَنَّةُ بِالْمَكَارِهِ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 6487]
المزيــد ...
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Moto umezingirwa na yenyekutamanisha, na Pepo imezingirwa na yenyekuchukiza".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 6487]
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Moto umezungukwa na kuzingirwa na mambo ambayo nafsi inayatamani, kama kufanya maharamisho au uzembe katika mambo ya wajibu; Atakayeendekeza matamanio ya nafsi yake katika hilo atastahiki moto, nakuwa Pepo imezungukwa na kuzingirwa na mambo ambayo yanachukiwa na nafsi; kama kudumu katika maamrisho na kuacha maharamisho na kuvumilia juu ya hilo, atakapovumilia na akapigana vita na nafsi yake juu ya hilo atastahiki kuingia Peponi.