عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنهما عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ:
«مَا يُصِيبُ الْمُسْلِمَ مِنْ نَصَبٍ وَلَا وَصَبٍ وَلَا هَمٍّ وَلَا حُزْنٍ وَلَا أَذًى وَلَا غَمٍّ حَتَّى الشَّوْكَةِ يُشَاكُهَا إِلَّا كَفَّرَ اللهُ بِهَا مِنْ خَطَايَاهُ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 5641]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Haumpati muislamu uchovu wala maradhi, wala msongo, wala huzuni, wala udhia, wala shida, hata mwiba unaomchoma, isipokuwa anamfutia Mwenyezi Mungu kupitia hilo makosa yake."
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 5641]
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yanayomsibu muislamu katika maradhi na msongo na huzuni na misukosuko na majanga na shida mbali mbali na hofu na njaa, hata kama utakuwa ni mwiba utakaomchoma na kumuumiza, hilo kwake linakuwa ni kafara ya madhambi kwake na kifuta makosa.