عَنْ طَلْحَةَ بْنِ عُبَيْدِ اللهِ رضي الله عنه قَالَ:
جَاءَ رَجُلٌ إِلَى رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ أَهْلِ نَجْدٍ ثَائِرُ الرَّأْسِ، نَسْمَعُ دَوِيَّ صَوْتِهِ، وَلَا نَفْقَهُ مَا يَقُولُ حَتَّى دَنَا مِنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَإِذَا هُوَ يَسْأَلُ عَنِ الْإِسْلَامِ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «خَمْسُ صَلَوَاتٍ فِي الْيَوْمِ وَاللَّيْلَةِ» فَقَالَ: هَلْ عَلَيَّ غَيْرُهُنَّ؟ قَالَ: «لَا، إِلَّا أَنْ تَطَّوَّعَ، وَصِيَامُ شَهْرِ رَمَضَانَ»، فَقَالَ: هَلْ عَلَيَّ غَيْرُهُ؟ فَقَالَ: «لَا، إِلَّا أَنْ تَطَّوَّعَ»، وَذَكَرَ لَهُ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الزَّكَاةَ، فَقَالَ: هَلْ عَلَيَّ غَيْرُهَا؟ قَالَ: «لَا، إِلَّا أَنْ تَطَّوَّعَ»، قَالَ: فَأَدْبَرَ الرَّجُلُ، وَهُوَ يَقُولُ: وَاللهِ، لَا أَزِيدُ عَلَى هَذَا، وَلَا أَنْقُصُ مِنْهُ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَفْلَحَ إِنْ صَدَقَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 11]
المزيــد ...
Kutoka kwa Twalha bin Ubeidi LLah -Radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutoka maeneo ya Najid, kichwa chake kikiwa kimetimka, tunasikia mvumo wa sauti yake, na wala hatuelewi anasema nini, mpaka akasogea karibu na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ghafla akaanza kuuliza kuhusu Uislamu, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Swala tano mchana na usiku" Akasema: Je kuna la wajibu juu yangu zaidi ya hayo? Akasema: "Hapana ila kama utajitolea" Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Na kufunga mwezi wa ramadhani" Akasema: Je kuna la wajibu juu yangu zaidi ya hilo? Akasema: "Hapana ila kama utajitolea" Akasema na akamtajia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- zaka, akasema: Je kuna la wajibu juu yangu zaidi ya hilo? Akasema: "Hapana ila kama utajitolea" Akageuka na kuondoka yule bwana huku akisema: Wallahi sitozidisha juu ya hayo wala sitopunguza, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Kafaulu ikiwa atakuwa mkweli".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 11]
Mtu mmoja miongoni mwa watu wa Najdi alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na nywele zake zikiwa zimetimkatimka na sauti yake ikiwa juu, wala haeleweki anasema nini, mpaka alipomkaribia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akauliza kuhusu faradhi za Uislamu?
Basi Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, akaanza na swala, na akamwambia kuwa Mwenyezi Mungu amemfaradhishia kuswali swala tano katika kila mchana na usiku.
Akasema: Je, ninalazimika kuswali swala zingine zaidi ya hizi tano?
Akasema: Hapana, labda kama utajitolea kuswali swala za sunna.
Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Na miongoni mwa ibada alizokuwajibishia Mwenyezi Mungu juu yako ni kufunga mwezi wa Ramadhani.
Yule bwana akasema: Je, ninalazimika kufunga funga zingine zaidi ya swaumu ya Ramadhani?
Akasema: Hapana, ila kama utajitolea kufunga.
Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamtajia Zaka
Yule bwana akasema: Je, ninalazimika chochote katika sadaka baada ya zaka ya faradhi?
Akasema: Hapana, ila kama utajitolea.
Baada ya mtu huyo kusikia faradhi hizo kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aligeuka na kuapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa atashikamana nazo bila ya kuongeza wala kupunguza, akasema rehema na amani zimshukie baada ya kauli yake hiyo: Ikiwa bwana huyu atakuwa mkweli kwa alichoapia, basi atakuwa miongoni mwa waliofaulu.