عن ابن مسعود رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم:
«الْجَنَّةُ أَقْرَبُ إِلَى أَحَدِكُمْ مِنْ شِرَاكِ نَعْلِهِ، وَالنَّارُ مِثْلُ ذَلِكَ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 6488]
المزيــد ...
Imepokelewa Kutoka kwa Ibn Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Pepo iko karibu mno kwa mmoja wenu kuliko umbali wa kanyagio la kiatu na kisigino chake, na moto pia hivyo hivyo".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 6488]
Alieleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Pepo na Moto viko karibu mno na mwanadamu kama ukaribu wa mwendo wa kiatu unaokuwa juu ya kisigino, kwa sababu anaweza kufanya twa'a (ibada) katika yale yanayomridhisha Allah Mtukufu akaingia Peponi kwa ibada hiyo, au dhambi moja likawa sababu ya kuingia motoni.