عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«الدُّنْيَا سِجْنُ الْمُؤْمِنِ وَجَنَّةُ الْكَافِرِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2956]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema: Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Dunia ni Gereza la Muumini na ni Pepo ya Kafiri".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2956]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba maisha ya Dunia kwa muumini ni kama Gereza analoishi kwa amri za kisheria, kama kufanya maamrisho na kuacha makatazo, basi akifa anapumzika na haya na anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu Mtukufu kwake, katika neema za kudumu, nayo kwa Kafiri ni kama Pepo; kwa sababu anafanya ndani yake kila inachotamani nafsi yake na kuamrishwa na matamanio yake, basi akifa anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama miongoni mwa adhabu za kudumu.