عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ مِنَ اللَّهِ، وَالحُلُمُ مِنَ الشَّيْطَانِ، فَإِذَا حَلَمَ أَحَدُكُمْ حُلُمًا يَخَافُهُ فَلْيَبْصُقْ عَنْ يَسَارِهِ، وَلْيَتَعَوَّذْ بِاللَّهِ مِنْ شَرِّهَا، فَإِنَّهَا لاَ تَضُرُّهُ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 3292]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Katada -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Ndoto njema hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ndoto mbaya hutoka kwa Shetani, atakapoota mmoja wenu ndoto mbaya anayoiogopa basi na ateme kushotoni kwake, na aombe ulinzi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari zake, kwani ndoto hiyo haitomdhuru".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 3292]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ndoto nzuri yenye kufurahisha usingizini hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na mtu kuota anayoyachukia na kumhuzunisha hutoka kwa Shetani.
Atakayeota yanayomchukiza basi ateme kushotoni kwake, na aombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake; kwani haitomdhuru, kiasi ambacho Mwenyezi Mungu amefanya hayo yaliyotajwa kuwa ni sababu ya kusalimika na hayo yenye kuchukiza yanayoambatana na ndoto.