عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ:
جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: السَّلَامُ عَلَيْكُمْ، فَرَدَّ عَلَيْهِ ثُمَّ جَلَسَ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «عَشْرٌ» ثُمَّ جَاءَ آخَرُ فَقَالَ: السَّلَامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ، فَرَدَّ عَلَيْهِ فَجَلَسَ، فَقَالَ: «عِشْرُونَ» ثُمَّ جَاءَ آخَرُ فَقَالَ: السَّلَامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ، فَرَدَّ عَلَيْهِ فَجَلَسَ، فَقَالَ: «ثَلَاثُونَ».
[حسن] - [رواه أبو داود والترمذي وأحمد والدارمي] - [سنن أبي داود: 5195]
المزيــد ...
Kutoka kwa Imran bin Huswaini radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Assalaam alaikum, akamjibu, kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kumi" Kisha akaja mwingine akasema: Assalaam alaikum warahmatullaah, akamjibu, akakaa, akasema: "Ishirini" Kisha akaja mtu mwingine akasema: Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh, akamjibu akakaa, akasema: "Thelathini".
[Ni nzuri] - - [سنن أبي داود - 5195]
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Assalaam alaikum" Akamjibu kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ameandikiwa mema kumi, kisha akaja mtu mwingine akasema: "Assalaam alaikum warahmatullaahi" Akamjibu, kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Amepata thawabu ishirini, kisha akaja mwingine akasema: "Assalaam alaikum warahmatullahi wabarakaatuh", akamjibu akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kapata thawabu thelathini; yaani kwa kila tamko ni mema kumi.