عن عائشة رضي الله عنها قالت: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«السِّوَاكُ مَطْهَرَةٌ لِلْفَمِ، مَرْضَاةٌ لِلرَّبِّ».

[صحيح] - [رواه النسائي وأحمد] - [مسند أحمد: 24203]
المزيــد ...

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Mswaki ni usafi wa kinywa, humridhisha Mola".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Nasai na Ahmad] - [Musnad wa Ahmad - 24203]

Ufafanuzi

Anatueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kusafisha meno kwa kijiti cha mti wa Arak na mfano wake husafisha kinywa kutokana na uchafu na harufu mbaya, Nakuwa ni katika sababu za kumridhisha Allah Mtukufu kwa mja; kwa sababu ndani yake kuna kumtii Allah na kuitika amri yake, na pia kuna usafi anaoupenda Allah Mtukufu.

Katika Faida za Hadithi

  1. Ubora wa mswaki, na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuuhimiza umma wake kukithirisha kupiga
  2. Katika mswaki ni bora kutumia kijiti cha mti wa Arak, na kutumia miswaki ya brashi na dawa ya meno hukaa badala yake.
Kuonyesha Tafsiri