عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ:
وُقِّتَ لَنَا فِي قَصِّ الشَّارِبِ، وَتَقْلِيمِ الْأَظْفَارِ، وَنَتْفِ الْإِبِطِ، وَحَلْقِ الْعَانَةِ، أَلَّا نَتْرُكَ أَكْثَرَ مِنْ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً.
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 258]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Tuliwekewa muda wa kupunguza sharubu, na kupunguza kucha, na kung'oa nywele za kwapa, na kunyoa nywele za siri, tusiziache zaidi ya siku arobaini.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 258]
Aliweka kikomo Mtume rehema na amani ziwe juu yake cha mtu kupunguza sharubu, na kupunguza kucha za mikono na miguu, na kung'oa nywele za kwapa, na kunyoa nywele za siri, kusizidi kuziacha kwake zaidi ya siku arobaini.