عن عائشة رضي الله عنها مرفوعاً: «عَشْرٌ من الفِطْرة: قَصُّ الشَارب، وإعْفَاء اللِّحْية، والسِّواك، وَاسْتِنْشَاقُ الماء، وقص الأظْفَار، وغَسْل البَرَاجِم، ونَتْف الإبْط، وحلق العَانة، وانْتِقَاصُ الماء» قال الراوي: ونَسِيْتُ العاشرة إلا أن تكون المَضْمَضَة. قال وكِيع - وهو أحد رواته - انْتِقَاص الماء: يعني الاسْتِنْجَاء.
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mambo kumi ni katika maumbile: Kupunguza masharubu, na kuziachia ndevu,na kupiga mswaki, na kupandisha maji puani, na kupunguza kucha, na kuosha fundo za vidole, na kunyofoa nywele za makwapani, na kunyoa nywele za sehemu za siri, na kustanji kwa maji". Anasema mpokezi : na nimelisahau la kumi nahisi huenda ikawa ni kusukutua. Amesema Wakii -naye ni mmoja kati ya wapokezi wake na kupunguza maji: Yaani kustanji.
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Anaeleza Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- jumla ya sunna za kimaumbile. Na "Maumbile" ni umbile ambalo Mwenyezi Mungu kawaumba viumbe juu yake, na akawafanya kuumbika (kulazimika) kulifanya, nakuwa hilo ni katika kheri na makusudio yake na ni umbile salama; kwasababu umbile lililopinda halizingatiwi; kwa kauli ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:"Kila mwenye kuzaliwa huzaliwa katika maumbile basi wazazi wake humfanya kuwa Yahudi au Mkristo au mmajusi". La kwanza: "kupunguza masharubu": kuyapunguza mpaka mdomo uonekane, kwa kile kinachopatikana ndani yake katika usafi, na kujilinda na vile vinavyotoka puani, kwani nywele za masharubu zinaposogea katika mdomo hugusa kile ambacho mdomo unakipata katika vyakula au vinywaji, na kuharibu muonekano pale zinapokithiri, hata kama atalipendezesha hilo asiyejali. Ni lazima muislamu achunge sharubu zake kwa kuzinyoa au kuzipunguza na asiziache zaidi ya siku arobaini; kwa yale aliyoyapokea Muslim kutoka kwa Anasi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-tuliwekewa muda sisi katika masharubu, na kupunguza kucha, na kukwapua nywele za kwapani, na kunyoa sehemu za siri, kuwa tusiziache zaidi ya siku arobaini" "Na kuziachia ndevu" Na ndevu: ni zile zilizoota katika kidevu au sharafa (nywele za shavuni), Na makusudio ya kuziachia: kuziacha zikiwa zimejaa asiziguse kwa kuzinyoa wala kuzipunguza,si kidogo wala kingi; kwasababu neno kuziachia limetokana na wingi na kujaza,kama kauli yake Mtukufu: (Mpaka walipoachilia), na zimekuja hadithi nyingi toka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- zikiamrisha kuzifuga kwa matamshi mengi; kwani imekuja kwa tamko:"jazeni ndevu" na kwa tamko:"Shusheni ndevu", na kwa tamko "Achieni ndevu", na kama inavyoonyesha amri ya kuziacha na kuzijaza na kutozigusa, na kwa msingi huu hairuhusiwi kwa muislamu kunyoa ndevu zake, ikiwa atafanya hivyo atakuwa kaenda kinyume na njia ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na atakuwa kaasi amri yake na kaangukia katika kujifananisha na makafiri."na mswaki" Yaani: katika mambo ya kimaumbile ambayo sheria imeyahimiza, Nikuwa "(mswaki) ni Kisafisha kinywa na humridhisha Mola" na ndio maana ni sheria kila wakati lakini inatiwa mkazo zaidi wakati wa udhu na swala na wakati wa kuamka toka usingizini na kubadilika kwa harufu ya mdomo, na meno kuwa ya njano na mfano wake. "na kupandisha maji puani" Yaani: nikuwa kupandisha maji ni katika maumbile, na kuondoa vilivyoko puani katika uchafu ambao unaweza kumsababishia udhia na madhara. Na kupandisha maji puani kunakuwa wakati wa udhu na kunakuwa nje ya udhu,kama mtu akihitaji kusafisha pua na kupandisha maji kwa kusafisha pua yake, na hii inatofautiana kulingana na watu, kuna baadhi ya watu hawahitaji hili isipokuwa katika udhu, na kuna watu wanalihitaji hili kwa wingi. Na miongoni mwa hilo pia: Yaani miongoni mwa sunna za maumbile ni kusukutua, kwani hilo ni katika maumbile; mdomo na pua mara nyingi vinazungukwa na uchafu, hivyo ikawa ni sehemu katika maumbile kuvizingatia."Na kupunguza kucha" Yaani katika mambo ya kimaumbile: ni kupunguza kucha, na makusudio yake ni kucha za mikono na miguu, zisiachwe zaidi ya siku arobaini; kwa mujibu wa hadithi iliyotangulia."Na kuosha fundo za mikono" Yaani na kuosha maungio ya vidole juu na ndani; kwasababu ni miongoni mwa sehemu unapokusanyikia uchafu; kwa kukunjamana kwake, hivyo huenda maji yasifike, na vikitiliwa umuhimu wa kuvisugua, na vikapitishwe tena mkono mara ya pili, basi maji yatavifikia, ikawa katika maumbile ni kuvitilia umuhimu. Na viunganishwe pamoja na fundo za vidole kila sehemu katika mwili inayokusanya uchafu kwa jasho au kinginecho kama mikunjo ya sikio na ndani ya mapaja na sehemu zinginezo zilizozidi kujikunja."Na kukwapua nywele za kwapani" Yaani: Katika mambo ya kimaumbile ni kukwapua nywele za kwapani, nako ni kuzivuta na kuzing'oa, na hiyo ni kwasababu ni sehemu inayokithiri jasho, na unakusanyika hapo uchafu, na harufu hubadilika, na zisiachwe zaidi ya siku arobaini; kwa kile kilichotangulia katika hadithi ya Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, na bora zaidi ni kuzinyofoa ikiwa ataweza, na ikiwa kunyofoa ni vigumu, basi hakuna tatizo kama atazinyoa na akatumia mafuta ya kuziondoa; kwasababu lengo ni kuziondoa na kusafisha mahali hapo, na tayari limefanyika."Na kunyoa sehemu za siri" Yaani: Katika mambo ya kimaumbile ni kuondoa nywele za sehemu ya siri, nazo ni nywele zinazoota sehemu ya siri ya mbele, kwa mwanaume na mwanamke, hivyo ni katika maumbile kuziondoa, sawa sawa iwe ni kwa kuzinyoa au kuzinyofoa au kuzipunguza au kwa kutumia vyombo vya kisasa; kwasababu lengo ni kusafisha, na tayari lengo limetimia, na wala asiziache kwa muda wa siku arobaini kwa hadithi ya Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Na kupunguza maji" Yaani ni katika maumbile kupunguza maji, na imefasiriwa kwa maana ya: kustanji, na inapewa nguvu maana hii kwa riwaya ya Abuudaudi na bin Majah kutoka Ammar bin Yaasir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:"Ni katika maumbile: Kusukutua, na kupandisha maji puani. Na kusafisha", Na kusatanji: ni kuondoa kilichotoka katika moja ya njia mbili kwa kitu kilichosafi, kama maji na jiwe na vitambaa, na mfano wa hivyo katika vile ambavyo vinahusika na kusafisha."Amesema mpokezi: Na nimesahau jambo la kumi, huenda likawa ni kusukutua "Hii ni shaka toka kwa mpokezi. Na uhakika wake nikuwa mambo haya yote, yanakamilisha muonekano wa mwanadamu na yanamsafisha na yanamtwaharisha, na yanamuondolea mambo yenye kumdhuru na machafu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama