عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«يَعْقِدُ الشَّيْطَانُ عَلَى قَافِيَةِ رَأْسِ أَحَدِكُمْ إِذَا هُوَ نَامَ ثَلاَثَ عُقَدٍ يَضْرِبُ كُلَّ عُقْدَةٍ عَلَيْكَ لَيْلٌ طَوِيلٌ، فَارْقُدْ، فَإِنِ اسْتَيْقَظَ فَذَكَرَ اللَّهَ، انْحَلَّتْ عُقْدَةٌ، فَإِنْ تَوَضَّأَ انْحَلَّتْ عُقْدَةٌ، فَإِنْ صَلَّى انْحَلَّتْ عُقْدَةٌ، فَأَصْبَحَ نَشِيطًا طَيِّبَ النَّفْسِ، وَإِلَّا أَصْبَحَ خَبِيثَ النَّفْسِ كَسْلاَنَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1142]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Anafunga shetani juu ya kisogo cha kichwa cha mmoja wenu, pindi anapolala, mafundo matatu, anafunga katika kila fundo usiku kucha na husema : basi lala, pindi anapoamka na akamtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu linafunguka fundo moja, akitawadha, linafunguka fundo jingine, na akiswali, yanafunguka mafundo yake yote, anaamka akiwa na uchangamfu na moyo mkunjufu, na vinginevyo basi anaamka akiwa na nafsi chafu tena mvivu".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1142]
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake hali ya shetani na mapambano yake na mwanadam anayetaka kusimama kwa ajili ya swala ya usiku au Alfajiri.
Muumini anapokwenda kulala shetani hufunga katika kisogo chake -yaani mwisho wa kichwa chake- mafundo matatu.
Muumini atakapoamka na akamtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akawa hajatii wasi wasi wa shetani; fundo moja hufunguka.
Akitawadha linafunguka fundo jingine. .....
Na ikiwa atasimama akaswali yatafunguka mafundo yote matatu, na atakuwa na uchangamfu wa nafsi; na kufurahi kwake kwa yale aliyoafikishwa na Mwenyezi Mungu katika ibada, akijipa bishara kwa yale aliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu katika thawabu na msamaha, ikiwa ni pamoja na hivyo vilivyomuondokea katika mafundo ya shetani na vikwazo vyake, na asipofanya hivyo atakuwa na nafsi chafu, atakuwa na moyo wenye huzuni, mvivu katika mambo ya kheri na mambo mema; kwa sababu atakuwa kafungwa kwa pingu za shetani, na atakuwa kawekwa mbali na kumkaribia Rahmani (Mwingi wa rehema).