عن أبي عبد الله ويقال أبو عبد الرحمن ثوبان مولى رسول الله صلى الله عليه وسلم رضي الله عنه قال: سمعت رسول لله صلى الله عليه وسلم يقول: «عليك بكثرة السجود؛ فإنك لن تسجد لله سجدة إلا رَفَعَكَ الله بها دَرَجة، وحَطَّ عنك بها خَطِيئة».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Abdillah na anaitwa Abuu Abdur Rahman Thauban kijana wa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Na Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akisema: "Shikamana na kukithirisha kusujudu; kwani wewe hutosujudu kwaajili ya Mwenyezi Mungu sijida moja isipokuwa atakunyanyua Mwenyezi Mungu kwa hiyo sijida daraja moja, na anakufutia kwa hiyo dhambi moja".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Sababu ya hadithi hii: Nikuwa Ma'dan bin Twalha Amesema: "Nilimwendea Thauban nikasema: Nieleze jambo ambalo nitalifanya aniingize peponi Mwenyezi Mungu kupitia hilo, Au alisema: Jambo linalopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu, akanyamaza, kisha akamuuliza akanyamaza, kisha akamuuliza mara ya tatu akasema: Nilimuuliza juu ya hilo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akasema: Ni juu yako, akalitaja jambo hilo, na mwisho wake: Nikakutana na Abuu dardaa nikamuuliza akaniambia mfano wa yale aliyoniambia Thauban". Na maana ya kauli yake -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Ni juu yako kukithirisha kusujudu" Maana yake: Shikamana na kukithirisha kusujudu, (kwani wewe hutosujudu kwaajili ya Mwenyezi Mungu sijida moja isipokuwa atakunyanyua daraja moja, na atakufutia kupitia hiyo kosa moja), Na hii ni kama hadithi ya Rabi'a bin Ka'b Al Aslamiy, Yakwamba yeye alisema kumwambia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: Nakuomba kuambatana na wewe peponi, Akasema: (Basi nisaidie wewe mwenyewe kwa nafsi yako kukithirisha kusujudu). Na kutoka kwa Ubada bin Swamit Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yakwamba yeye alimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake akisema: (Hakuna mja atakayesujudu kwaajili ya Mwenyezi Mungu sijida moja isipokuwa Mwenyezi Mungu atamuandikia kupitia sijida hiyo jema moja, na atamfutia dhambi moja na atamnyanyua kwa hiyo daraja moja, hivyo takeni ziada katika kusujudu). Hivyo kusujudu kwaajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni katika utiifu bora, na ibada tukufu; kwa kile kilichomo miongoni mwa unyenyekevu wa hali ya juu na utumwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ndani yake kuna kukituliza kiungo kitukufu zaidi cha mwanadamu na cha juu ambacho ni kichwa chake katika udongo unaokanyagwa na kudhalilishwa. Kisha makusudio ya kusujudu hapa ni kile kinachoambatana na swala, si sijida pekee; kwasababu hiyo haifai kwa kukosekana ushahidi unaojulisha hilo kisheria; na msingi katika ibada ni kutofanya, isipokuwa ile itakayokuwa na sababu nayo ni sijida ya kisomo au sijida ya shukurani sheria ilizileta hizo. Kisha akabainisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yale anayoyapata mtu katika malipo pale anapokuwa kasujudu; nayo ni kuwa anapata faida mbili: Faida ya kwanza: Nikuwa Mwenyezi Mungu anamnyanyua kwa hiyo daraja moja, yaani nafasi huko kwake na katika nyoyo za watu, na hivyo hivyo katika matendo yako mazuri, anakunyanyua Mwenyezi Mungu kupitia hayo daraja. Na faida ya pili: Nikuwa anakufutia kupitia hiyo dhambi, na mwanadamu hupatikana kwake ukamilifu pale yanapoondoka anayoyachukia, na kupata yale anayoyapenda, hivyo kunyanyuliwa daraja ni katika mambo anayoyapenda mwanadamu, na makosa ni miongoni mwa yale anayoyachukia mwanadamu, hivyo akinyanyuliwa daraja na akafutiwa kupitia hayo makosa; basi lengo atakuwa kalipata, na atakuwa kasalimika na yale yenye kumuogopesha.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri
Kuonyesha Tarjama