+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ:
كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَسِيرُ فِي طَرِيقِ مَكَّةَ، فَمَرَّ عَلَى جَبَلٍ يُقَالُ لَهُ جُمْدَانُ، فَقَالَ: «سِيرُوا هَذَا جُمْدَانُ، سَبَقَ الْمُفَرِّدُونَ» قَالُوا: وَمَا الْمُفَرِّدُونَ يَا رَسُولَ اللهِ؟ قَالَ: «الذَّاكِرُونَ اللهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتُ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2676]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akitembea katika njia ya kuelekea Makka, akapita karibu na mlima Jumdan, akasema: “Tembeeni huu ni mlima Jumdan, Wamepata ushindi wenye kujitenga” Wakasema: Ni akina nani hao wenye kujitenga ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Ni wenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi katika Wanaume, na wenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi katika wanawake.”

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2676]

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameeleza nafasi ya wale wanaomkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na kwamba wao ni wa kipekee na wametangulia wengine katika kufikia daraja za juu katika Bustani za neema, na akawafananisha na mlima Jumdan ambao ni wa kipekee ukilinganisha na milima mingine.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية الموري Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Inapendeza kufanya dhikiri kwa wingi, na kushughulishwa nayo, kwa sababu kutangulia huko Akhera kunapatikana kupitia vitendo vingi vya utii na ikhlasi katika ibada.
  2. Kumtaja Mwenyezi Mungu kunaweza kuwa kwa ulimi tu, au kwa moyo tu, au kwa ulimi na moyo pamoja ambayo ni kiwango cha juu zaidi.
  3. Miongoni mwa dhikiri ni nyiradi za kisheria ambazo zimewekewa mipaka, kama vile dhikiri za asubuhi na jioni, na za baada ya sala za faradhi, na nyinginezo.
  4. Amesema Al-Nawawi: Tambua kuwa fadhila za dhikiri hazikomei katika kumtukuza Mwenyezi Mungu (Tasbiih), na tahalil (Laa ilaaha illa llaah), na kumsifu (Tahmiid), na takbir (Allahu Akbar) na mengineyo, bali kila mwenye kumtii Mwenyezi Mungu basi huyo anamdhukuru Mwenyezi Mungu.
  5. Ameeleza Mwenyezi Mungu kuwa miongoni mwa sababu kubwa za kupewa uimara (Thabati), akasema Mtukufu: "Enyi mlio amini! Mkikutana na jeshi, basi kueni imara, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu sana ili mpate kufanikiwa." [Al-Anfaal:45].
  6. Sababu ya kufananisha kati ya wanaomtaja Mwenyezi Mungu na Mlima Jumdan ni upekee wake na kujitenga kwake. Mlima Jumdan umejitenga na milima mingine, hivyo hata wanaomkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu wamejitenga pia, mwenye kujitenga ni yule ambaye moyo wake na ulimi wake viko peke yake kwa kumkumbuka Mola wake Mlezi, hata akiwa miongoni mwa watu, na anapata faraja kwa nyakati anazojitenga, na anapata upweke nyakati anazokuwa na watu wengi. Na inaweza kuwa sababu ya kufananishwa mfano huo ni kuwa dhikiri ndio sababu ya uthabiti katika dini kama vile milima ni sababu ya kuimarika kwa ardhi, au ni kwakuwa anakuwa yeye ndiye wa kwanza kupata amali njema duniani na Akhera, kwa sababu msafiri anayetoka Madina kwenda Makka alikuwa anapofika Jumdan, ni dalili ya kuwa kafika Makka, na mwenye kuufikia anakuwa ndiye wa kwanza, basi hivyo hivyo mwenye kumdhukuru Mwenyezi Mungu yuko mbele ya wengine kwa kumkumbuka kwake Mwenyezi Mungu kwa wingi, na Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi.