عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«رَغِمَ أَنْفُ، ثُمَّ رَغِمَ أَنْفُ، ثُمَّ رَغِمَ أَنْفُ»، قِيلَ: مَنْ؟ يَا رَسُولَ اللهِ قَالَ: «مَنْ أَدْرَكَ أَبَوَيْهِ عِنْدَ الْكِبَرِ، أَحَدَهُمَا أَوْ كِلَيْهِمَا فَلَمْ يَدْخُلِ الْجَنَّةَ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2551]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Ameangukia pua (kapata hasara), kisha Ameangukia pua (kapata hasara), kisha Ameangukia pua (kapata hasara), atakayewakuta wazazi wake wawili wakati wa utuuzima, mmoja wao au wote wawili, na akawa hakuingia peponi".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2551]
Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliomba dua ya udhalili na fedheha mpaka akahisi kana kwamba mtu ametia pua yake kwenye mchanga – akarudia mara tatu – akaulizwa: Ni nani huyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, uliyemuombea dua mbaya?
Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Atakayewakuta wazazi wake wawili, mmoja wao au wote wawili, wakati wa utuuzima, wakawa si sababu ya yeye kuingia Peponi; na hii ni kutokana na kukosa kuwatendea wema na kutowatii.