عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: ثَلاَثَةٌ أَنَا خَصْمُهُمْ يَوْمَ القِيَامَةِ: رَجُلٌ أَعْطَى بِي ثُمَّ غَدَرَ، وَرَجُلٌ بَاعَ حُرًّا فَأَكَلَ ثَمَنَهُ، وَرَجُلٌ اسْتَأْجَرَ أَجِيرًا فَاسْتَوْفَى مِنْهُ وَلَمْ يُعْطِهِ أَجْرَهُ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 2270]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Watu wa aina tatu mimi ndiye mgomvi wao siku ya Kiyama: Mtu aliyetoa (kiapo) kwa jina langu kisha akafanya usaliti, na mtu aliyemuuza mtu huru kisha akala thamani yake, na mtu aliyempa kazi mwajiriwa, akatimiza majukumu yake na hakumpa malipo yake".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 2270]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Watu wa aina tatu mimi ndiye nitakayepambana nao siku ya Kiyama, na nitakayekuwa mgomvi wake basi nitapambana naye na kumshinda: Wa kwanza: Atakayetoa kiapo na akaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, na akachukua ahadi kisha akaitengua na kufanya hiana. Wa pili: Atakayemuuza mtu huru kwa kumfanya kuwa mtumwa na akala thamani yake na akakitumia kiwango cha pesa aliyopata. Wa tatu: Atakayemuajiri muajiriwa katika kazi, akamtimizia kazi yake na hakumpa thamani ya kazi yake.