+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«تَهَادَوا تَحَابُّوا».

[حسن] - [رواه البخاري في الأدب المفرد وأبو يعلى والبيهقي] - [الأدب المفرد: 594]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- anasema:
"Peaneni zawadi, mtapendana."

[Ni nzuri] -

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemhimiza Muislamu kuwa abadilishane zawadi na ndugu yake Muislamu, na kuwa zawadi ni miongoni mwa sababu za mapenzi na kuziunganisha nyoyo.

Katika Faida za Hadithi

  1. Ni sunna kutoa zawadi; kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameamrisha kufanya hivyo.
  2. Zawadi ni sababu ya kuleta mapenzi.
  3. Inampasa mwanadamu afanye kila ambacho ndani yake kinaleta mapenzi kati yake na watu wengine, sawa sawa iwe ni katika zawadi au kuwa mpole, au katika maneno mazuri au katika ukunjufu wa uso kwa kadiri awezavyo.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiindonesia Kibangali Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai Kiassam الهولندية الغوجاراتية الدرية المجرية الجورجية المقدونية
Kuonyesha Tarjama