+ -

عَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ:
بَعَثَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَرِيَّةً فَاسْتَعْمَلَ رَجُلًا مِنَ الأَنْصَارِ، وَأَمَرَهُمْ أَنْ يُطِيعُوهُ، فَغَضِبَ، فَقَالَ: أَلَيْسَ أَمَرَكُمُ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ تُطِيعُونِي؟ قَالُوا: بَلَى، قَالَ: فَاجْمَعُوا لِي حَطَبًا، فَجَمَعُوا، فَقَالَ: أَوْقِدُوا نَارًا، فَأَوْقَدُوهَا، فَقَالَ: ادْخُلُوهَا، فَهَمُّوا، وَجَعَلَ بَعْضُهُمْ يُمْسِكُ بَعْضًا، وَيَقُولُونَ: فَرَرْنَا إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنَ النَّارِ، فَمَا زَالُوا حَتَّى خَمَدَتِ النَّارُ، فَسَكَنَ غَضَبُهُ، فَبَلَغَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: «لَوْ دَخَلُوهَا مَا خَرَجُوا مِنْهَا إِلَى يَوْمِ القِيَامَةِ؛ الطَّاعَةُ فِي المَعْرُوفِ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 4340]
المزيــد ...

Imesimuliwa kutoka kwa Ali, Mwenyezi Mungu amridhie, kwamba alisema:
Alituma kikosi Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuweka kiongozi bwana mmoja katika Maanswari (watu wa Madina), na akawaamrisha wamtii, akachukia, akasema: Hivi hakukuamrisheni Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mnitii? Wakasema: Ndivyo, akasema: Nikusanyieni kuni, wakakusanya, akasema: Niwashieni moto, wakauwasha, akasema: Ingieni humo, wakataka kuuingia, baadhi yao wakaanza kuwashika wenzao, huku wakisema: Tumeukimbia moto tukaelekea kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, waliendelea katika hali hiyo mpaka moto ukazima, zikatulia hasira zake, habari zikamfikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Laiti wangeingia wasingelitoka humo mpaka siku ya Kiyama; Utiifu unakuwa katika jambo jema".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 4340]

Ufafanuzi

Alituma Jeshi Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akamfanya bwana mmoja katika Maanswari kuwa kiongozi wao, na akawaamrisha wamtii, yule kiongozi akawakasirikia na akasema kuwaambia: Hivi hakuwaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mnitii? Wakasema: Hasa! akasema: Basi nimekuamrisheni nikusanyieni kuni na muwashe moto kisha muingie humo, wakakusanya kuni na wakawasha moto, walipotaka kuingia humo, wakaanza kutazamana wao kwa wao. Na wakasema: Hakika sisi hatukumfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake ila ni kwa sababu ya kuukimbia moto, je, tuuingie? wakiwa bado wako katika hali hiyo muwako wa moto ukazimika, na ikatoweka kwa kiongozi ghadhabu yake. Akaelezwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu hilo akasema: Lau wangelimtii na wakaingia katika moto waliouwasha basi wangeliadhibiwa humo na wasingetoka kamwe kwa muda wa kubakia dunia, hakuna kumtii kiumbe katika kumuasi muumba; bali utiifu ni wajibu katika mambo mema na si katika maasi.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa kuwa utiifu unakuwa katika mema na wala hauwi katika maasi, hata kama amri itatoka kwa mtu ambaye ni wajibu kumtii.
  2. Mtenda maasi mwenye tauhidi ameahidiwa moto, lakini pia Mwenyezi Mungu anaweza kumsamehe.
  3. Sheria ya kuweka kiongozi vitani, na vile vile safarini.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiindonesia Kibangali Kivetenamu Kikurdi Kihausa Kireno Thai Kiassam الهولندية الغوجاراتية الدرية المجرية الجورجية المقدونية
Kuonyesha Tarjama