+ -

عَنْ أُمَيْمَةَ بِنْتِ رُقَيْقَةَ رضي الله عنها أَنَّهَا قَالَتْ:
أَتَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي نِسْوَةٍ مِنَ الْأَنْصَارِ نُبَايِعُهُ، فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، نُبَايِعُكَ عَلَى أَلَّا نُشْرِكَ بِاللَّهِ شَيْئًا، وَلَا نَسْرِقَ، وَلَا نَزْنِيَ، وَلَا نَأْتِيَ بِبُهْتَانٍ نَفْتَرِيهِ بَيْنَ أَيْدِينَا وَأَرْجُلِنَا، وَلَا نَعْصِيَكَ فِي مَعْرُوفٍ، قَالَ: «فِيمَا اسْتَطَعْتُنَّ، وَأَطَقْتُنَّ» قَالَتْ: قُلْنَا اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَرْحَمُ بِنَا، هَلُمَّ نُبَايِعْكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنِّي لَا أُصَافِحُ النِّسَاءَ، إِنَّمَا قَوْلِي لِمِائَةِ امْرَأَةٍ كَقَوْلِي لِامْرَأَةٍ وَاحِدَةٍ، أَوْ مِثْلُ قَوْلِي لِامْرَأَةٍ وَاحِدَةٍ».

[صحيح] - [رواه الترمذي والنسائي وابن ماجه] - [سنن النسائي: 4181]
المزيــد ...

Kutoka kwa Umaima binti Ruqaiqa radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alisema:
Nilikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa katika kundi la wanawake ili wampe ahadi ya utiifu (Baiaa) wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tunakupa ahadi juu ya kutomshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na tusizini, na tusilete uzushi tutakaouzua mbele ya mikono yetu na miguu, na wala tusikuasi katika jema lolote, akasema: "Katika yale mnayoyaweza, na mkayahimili" Anasema: Tukasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanahuruma zaidi kwetu, njoo tukupe ahadi ya utiifu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika mimi siwapi mkono wanawake, bali hakika kauli yangu kwa wanawake mia moja ni sawa na kauli yangu kwa mwanamke mmoja, au ni mfano wa kauli yangu kwa mwanamke mmoja".

[Sahihi] - - [سنن النسائي - 4181]

Ufafanuzi

Ameeleza Umaima binti Ruqaiqa radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba yeye alimuendea Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa pamoja na wanawake wa ki Answari (watu wa Madina) wampe ahadi ya utiifu juu ya kutomshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na wala wasiibe, na wala wasizini, na wala wasilete uzushi watakaouzua mbele ya mikono yao na miguu yao, na wala wasimuasi katika jema lolote, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Katika yale mnayoyaweza, na mkayamudu. Tukasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanahuruma zaidi kweli, njoo tukupe ahadi ya utiifu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa kukupa mkono kama wanavyofanya wanaume, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika mimi siwapi mkono wanawake, bali kauli yangu na kukubali kwangu kuungwa mkono na wanawake mia moja ni sawa na kauli yangu kwa mwanamke mmoja.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa namna ya kumpa ahadi ya utiifu Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa wanawake.
  2. Uharamu wa kuwapa mkono wanawake wasiokuwa ndugu walioharamishwa kuwaoa.
  3. Majukumu ya kisheria yamefungamanishwa na uwezo na kumudu.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiindonesia Kisin-hala Kivetenamu Kihausa Thai Kiassam الهولندية الغوجاراتية الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama