عن سليمان بن صُرَدٍ رضي الله عنه قال: كنت جالسًا مع النبي صلى الله عليه وسلم ورجلان يَسْتَبَّانِ، وأحدهما قد احْمَرَّ وجْهُه، وانْتَفَخَتْ أَوْدَاجُهُ، فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «إِنِّي لأعلم كلمة لو قالها لذهبَ عنه ما يجد، لو قال: أعُوذ بالله من الشَّيطان الرجيم، ذهبَ منه ما يَجد». فقالوا له: إن النبي - صلى الله عليه وسلم - قال: «تَعَوَّذْ بالله من الشيطان الرجيم».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Suleiman bin Suradi- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Nilikuwa nimekaa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na kukiwa na watu wawili wanatukanana, na mmoja wao ukiwa tayari uso wake umekuwa mwekundu, na mishipa yake imesimama, akasema: Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Hakika mimi ninajua neno ambalo laiti angelisema yangemuondokea yaliyompata, lau angelisema: Au'dhubillaahi minshaitwanir-rajiim, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shetani aliyelaaniwa, yangemuondokea yaliyompata" Wakasema kumwambia: Hakika Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- amesema: "Jikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shetani aliyelaaniwa".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Anaeleza Suleiman bin Suradi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa watu wawili walitukanana mbele ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, akachukia mmoja wao na hasira yake ikapanda mpaka ukaumuka uso wake na akabadilika, Akasema Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake-: Hakika mimi ninajua neno lau angelisema basi yangeondoka kwake anayoyapata miongoni mwa hasira, lau angesema: Au'dhubillaahi minashaitwanir rajiim; Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shetani aliyelaaniwa; kwasababu yaliyompata yametokana na shetani, anapojikinga mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na akajielekeza kwake kutokana na shari za shetani, Mwenyezi Mungu humuondoshea yale anayoyapata katika hasira, kwa baraka za neno hili, wakasema kumwambia yule bwana: Hakika Nabii amesema: sema: Au'dhubillaahi minashaitwanir rajiim -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shetani aliyelaaniwa. katika baadhi ya riwaya huyu bwana hakuweza kusema kutokana na hasira kali aliyokuwa nayo bali alisema: kwani mimi nimechanganyikiwa?.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kireno
Kuonyesha Tarjama