عن أبي الدَّرْدَاء رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «ألا أُنَبِّئُكُمْ بِخَيْرِ أعْمَالِكُم، وأزْكَاها عند مَلِيكِكُم، وأرْفَعِهَا في دَرَجَاتِكُمْ، وخير لكم من إنْفَاق الذهب والفضة، وخير لكم من أن تَلْقَوا عَدُوَّكُمْ فَتَضْرِبُوا أعْنَاقَهُمْ ويَضْرِبوا أعْنَاقَكُم؟» قالوا: بلى، قال: «ذكر الله تعالى ».
[صحيح] - [رواه الترمذي وأحمد وابن ماجه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Dardaa -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Je nikujulisheni matendo yenu bora, na matukufu mbele ya mfalme wenu, na yanayonyanyua zaidi katika daraja zenu, na ni bora zaidi kwenu kuliko kutoa dhahabu na fedha, na ni bora hata kuliko kukutana adui mkapiga shingo yake na akapiga shingo zenu" wakasema: Tueleze, Akasema: "Ni kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu".
Sahihi - Imepokelewa na Ibnu Maajah

Ufafanuzi

Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Je nikuelezeni matendo bora kwenu, na yenye thawabu nyingi na mazuri zaidi kwa Mola wenu, na yanayonyanyua zaidi daraja zenu, na ni bora kwenu kuliko kutoa dhahabu na fedha katika njia ya Mwenyezi Mungu, na ni bora kwenu kuliko kukutana na makafiri katika viwanja vya vita mkapiga shingo zao kwaajili ya kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu Mtukufu. Wakasema maswahaba: Tueleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Akasema: Ni kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno الدرية
Kuonyesha Tarjama