عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«أَلَا أَدُلُّكُمْ عَلَى مَا يَمْحُو اللهُ بِهِ الْخَطَايَا، وَيَرْفَعُ بِهِ الدَّرَجَاتِ؟» قَالُوا بَلَى يَا رَسُولَ اللهِ قَالَ: «إِسْبَاغُ الْوُضُوءِ عَلَى الْمَكَارِهِ، وَكَثْرَةُ الْخُطَا إِلَى الْمَسَاجِدِ، وَانْتِظَارُ الصَّلَاةِ بَعْدَ الصَّلَاةِ، فَذَلِكُمُ الرِّبَاطُ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 251]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Je! nikujulisheni mambo ambayo yakifanyika Allah hufuta madhambi na hupandisha daraja kwa mambo hayo?" wakasema: Ndiyo, ewe Mtume wa Allah, akasema: "Kutawadha vizuri wakati wa baridi, na kuzidisha hatua kwenda msikitini, na kusubiria swala baada ya swala huko ndiko kuizuia nafsi katika mambo ya kheri."
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 251]
Mtume rehema na amani ziwe juu yake, aliwauliza maswahaba zake iwapo wanataka awaongoze katika matendo yatakayowapelekea kupata msamaha wa madhambi, na kufutwa kwake kutoka katika vitabu vya Malaika wenye kuhifadhi, na kupata daraja za juu Peponi?
Maswahaba wakasema: Ndio tunataka hivyo. Akasema:
Ya kwanza: Kueneza na kukamilisha udhu kwa shida; kama vile baridi, ukosefu wa maji, na maumivu ya mwili, na maji ya moto.
Pili: Kupiga hatua nyingi - ambazo ni kati ya miguu miwili- kwenda misikiti iliyo mbali na nyumbani, na kurudi rudi kila wakati.
Tatu: Kungoja wakati wa Swala, na moyo kuambatana nayo, na kujitayarisha kwa ajili yake, na kukaa msikitini kwa ajili yake kungojea jamaa, anaposwali hungojea mahali pake pa kuswali kwa ajili ya swala nyingine.
Kisha akaeleza rehema na amani ziwe juu yake kuwa mambo haya ndiyo Jihadi ya kweli; Kwa sababu yanaziba njia za Shetani juu ya nafsi, na yanatenza nguvu matamanio, na yanaizuia isiingiwe na wasi wasi, hivyo kundi la Mwenyezi Mungu likashinda majeshi ya Shetani kupitia hayo; na hii ndiyo Jihadi kubwa zaidi, kwakuwa imekuwa kama kikosi cha jeshi upande wa maadui.