+ -

عن حارثة بن وهب رضي الله عنه مرفوعًا: «ألا أُخْبِركم بأهل الجنة؟ كلُّ ضعيفٍ مُتَضَعَّفٍ، لو أقسم على الله لَأَبَرَّهُ، ألا أُخْبِركم بأهل النار؟ كُلُّ عُتُلٍّ جَوَّاظٍ مُسْتَكْبِرٍ».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Haritha bin Wahabi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Hivi nisikuelezeni watu wa peponi? Kila mnyonge mwenye kujishusha, na lau kama angeliapia kwa Mwenyezi Mungu basi angelimuepusha na kila linalompa uzito, Hivi nisikuelezeni watu wa motoni? kila jeuri mkali mwenye kiburi".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Miongoni mwa sifa za baadhi ya watu wa peponi; Nikuwa mtu anakuwa mnyonge mwenye kujishusha, Yaani: Hajali cheo au nafasi yake, au akafanya pupa ya kupata vyeo vya juu duniani, lakini yeye ni mnyonge ndani ya nafsi yake na anakuwa mnyonge kwa mwingine, na lau angeliapa kwa jambo lolote basi Mwenyezi Mungu angemfanyia jambo lake kuwa jepesi, ili amtimizie yale aliyoyaapia, ama watu wa motoni miongoni mwao ni kila mkali mwenye tabia ngumu msusuavu asiyetii haki, na kila mwenye kukusanya mali na akazuia kutoa yale ya wajibu ndani yake katika zaka, na mwenye kuikataa haki kwa kiburi na akajikweza kwa watu, na hadithi haimaanishi ni hawa tu, bali ni kwaajili ya kubainisha baadhi ya sifa za makundi mawili.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama