عن عبد الله بن عمر -رضي الله عنهما- عن النبي -صلى الله عليه وسلم-قال: «من تَشبَّه بقوم, فهو منهم».
[حسن.] - [رواه أبو داود وأحمد.]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdallah bin Omar Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: Amesema: "Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni miongoni mwao".
Ni nzuri - Imepokelewa na Abuu Daud

Ufafanuzi

Hadithi inamaanisha ujumla, atakayejifananisha na watu wema basi atakuwa mwema na atafufuliwa pamojanao, na atakayejifananisha na makafiri au waovu basi na yeye atakuwa katika njia yao na mfumo wao.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu
Kuonyesha Tarjama
1: Tahadhari ya kutojifananisha na makafiri.
2: Kuhimizwa juu ya kujifananisha na watu wema.
3: Nyenzo huchukua hukumu ya malengo yake, kujifananisha katika muonekano huleta mapenzi kiundani.
4: Hukumu za kujifananisha ziko katika ufafanuzi, haiwezekani kuzikusanya zote, kwasababu zinatofautiana kulingana na aina ya kujifananisha na madhara yanayoambatana na hilo, hasa hasa katika zama hizi, bali ni lazima kuyaleta mambo yote katika ushahidi wa kisheria.
5: Katazo la kujifananisha na makafiri bila shaka ni katazo la kujifananisha nao katika dini yao, na katika tamaduni zao ambazo ni maalumu kwao, ama yatakayekuwa kinyume na hivyo kama kujifunza ufundi na mfano wake hayaingii katika katazo hili.