عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعاً: «ليس الشديد بالصُّرَعة، إنما الشديد الذي يملك نفسه عند الغضب».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Hadithi Marfu'u: "Hawi mtu mkali kwa miereka, hakika mkali ni yule anayemiliki nafsi yake wakati wa hasira".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Nguvu za kiuhalisia si hizi nguvu za viungo vya mwili, na wala mkali mwenye nguvu si yule anayewapiga miereka wengine siku zote, bali mwenye nguvu na mkali ni yule aliyepambana na nafsi yake na akaitenza nguvu pale ambapo inapozidiwa na hasira; kwasababu hili linaonyesha juu ya nguvu yake ya kuweza kujimiliki na kumzidia kwake shetani.