عن أبي ذر الغفاري رضي الله عنه مرفوعاً: «لا تَحْقِرَنَّ من المعروف شيئا، ولو أن تَلْقَى أخاك بوجه طَلْق».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Dhari Al-Ghifariy- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Usidharau kabisa katika wema kitu chochote, hata kama ni kukutana na ndugu yako kwa uso mkunjufu".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Hadithi inaonyesha juu ya kupendeza kuwa na uso mkunjufu wakati wa kukutana, nakuwa hili ni katika wema ambao inampasa muislamu aupupie na wala asiudharau, kwakuwa ndani yake kuna kumliwaza ndugu muislamu na kuingiza furaha kwake.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese German Kijapani
Kuonyesha Tarjama

Faida nyingi

  1. Kutafuta kupendana baina ya waumini, na ukunjufu wa uso na kutabasamu kwake na bashasha.
  2. Ukamilifu wa sheria hii na kuenea kwake, nakuwa imekuja na mambo yote ambayo ndani yake kuna kutengemaa kwa waislamu na kufanya neno lao kuwa ni moja.
  3. Kupupia juu ya kufanya mema hasa hasa yale yanayohusiana na watu wengine, na wala asidharau katika wema lolote.
  4. Kupendeza (ni sunna) kuingiza furaha kwa waislamu; kwa yale yanayopatikana ndani yake kama kudumisha huruma baina yao.