+ -

عن عائشة رضي الله عنها قالت:
سَأَلَ أُنَاسٌ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الْكُهَّانِ، فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَيْسُوا بِشَيْءٍ» قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، فَإِنَّهُمْ يُحَدِّثُونَ أَحْيَانًا بِالشَّيْءِ يَكُونُ حَقًّا، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «تِلْكَ الْكَلِمَةُ مِنَ الْحَقِّ يَخْطَفُهَا الْجِنِّيُّ فَيَقُرُّهَا فِي أُذُنِ وَلِيِّهِ قَرَّ الدَّجَاجَةِ، فَيَخْلِطُونَ فِيهَا أَكْثَرَ مِنْ مِائَةِ كَذْبَةٍ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6213]
المزيــد ...

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Kuna watu walimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu makuhani, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hawana lolote" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika wao husimulia jambo baadhi ya nyakati na likawa kweli, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Neno hilo huwa limetoka katika ukweli, Jini hulikwapua na kulinong'oneza katika sikio la kipenzi chake mfano wa kuku anavyotetea, hulichanganya na uongo zaidi ya mia moja (100)".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 6213]

Ufafanuzi

Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu wale wanaoeleza mambo yajayo yaliyofichikana, akasema: Msiwajali, na wala msiyachukue maneno yao, na wala msiyajali mambo yao.
Wakasema: Hakika kauli yao huendana na uhalisia katika baadhi ya nyakati, kama ambavyo huelezea kutokea kwa jambo la gahibu ndani ya mwezi fulani siku fulani, na likatokea sambamba na kauli yao.
Akasema -Rehema na amani ziwe juu yake-: Hakika Majini huiba yale wanayoyasikia katika habari za mbinguni, wakashuka kuja kwa watu wao miongoni mwa makuhani wakawaeleza waliyoyasikia, kisha kuhani anaongeza katika yale aliyoyasikia kutoka mbinguni uongo mia moja (100).

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Katazo la kuwasadikisha makuhani, nakuwa wanayoyasema ni uongo na uzushi, hata kama watasema ukweli katika baadhi ya nyakati.
  2. Mbingu zimehifadhiwa dhidi ya Mashetani kwa kutumwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ili wasije kusikiliza chochote katika wahyi au kinginecho, isipokuwa atakayeiba kusikiliza na akasalimika na kupigwa kimondo.
  3. Majini hujifanyia vipenzi katika binadamu.
Ziada