عن عمر رضي الله عنه قال: نُهِيَنا عن التَّكَلُّف.
[صحيح] - [رواه البخاري]
المزيــد ...

Kutoka kwa Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Tumekatazwa kujilazimisha.
Sahihi - Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Ufafanuzi

Anaeleza Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- katika hadithi hii kuwa wao "walikatazwa kujilazimisha" na mkatazaji ni Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake-; kwasababu swahaba anaposema: "Tumekatazwa" tamko hili linakuwa na hukumu ya kupelekwa moja kwa moja kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Yaani ni kama vile amesema: Ametukataza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kujilazimisha. Na kujilazimisha: Ni kila kitendo au kauli ambayo anatafuta mfanyaji wake kuonekana mbele ya wengine lakini hana uwezo huo. Mfano wa kauli: Kukithirisha maswali, na kutafuta mambo yenye kutatiza ambayo si lazima kuyatafuta, na kuchukua dhahiri ya sheria na kukubali yale yaliyoletwa na sheria, Na kutoka kwa Anasi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - Amesema: Tulikuwa kwa Omar na alikuwa na kanzu ambayo nyuma yake ilikuwa na michoro minne, akasoma aya: "Na matunda na malisho" Akasema: Haya matunda tunayajua, ni nini malisho? kisha akasema: "Tumekatazwa kujilazimisha". Na kitendo: kama mtu kupata mgeni kisha akajilazimisha kwa mambo ambayo ni magumu kwake, bali na huenda hilo likampelekea katika kudaiwa, na huenda asiweze kulilipa deni hilo, akajibebesha madhara duniani na Akhera. Ni juu ya muislamu kutojilazimisha katika mambo, bali ayafanye mambo kuwa kati na kati, kama ilivyokuwa hali yake Rehema na Amani ziwe juu yake- Hakibanii kilichopo wala hajilazimishi kisichokuwepo.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Kijapani
Kuonyesha Tarjama

Faida nyingi

  1. Katazo la kujilazimisha, na himizo la kujiweka mbali na hilo katika kila kitu.