+ -

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ:
بَيْنَمَا نَحْنُ فِي الْمَسْجِدِ مَعَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذْ جَاءَ أَعْرَابِيٌّ، فَقَامَ يَبُولُ فِي الْمَسْجِدِ، فَقَالَ أَصْحَابُ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: مَهْ مَهْ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا تُزْرِمُوهُ، دَعُوهُ» فَتَرَكُوهُ حَتَّى بَالَ، ثُمَّ إِنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ دَعَاهُ فَقَالَ لَهُ: «إِنَّ هَذِهِ الْمَسَاجِدَ لَا تَصْلُحُ لِشَيْءٍ مِنْ هَذَا الْبَوْلِ، وَلَا الْقَذَرِ إِنَّمَا هِيَ لِذِكْرِ اللهِ عَزَّ وَجَلَّ، وَالصَّلَاةِ وَقِرَاءَةِ الْقُرْآنِ» أَوْ كَمَا قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: فَأَمَرَ رَجُلًا مِنَ الْقَوْمِ فَجَاءَ بِدَلْوٍ مِنْ مَاءٍ فَشَنَّهُ عَلَيْهِ.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 285]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Siku moja sisi tukiwa Msikitini pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake ghafla akaja bedui, akasimama akaanza kukojoa Msikitini, wakasema Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Koma, koma!, anasema: Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Msimkatishe, muacheni" Wakamuacha mpaka akamaliza kukojoa, kisha baada ya hapo Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuita, akasema kumuambia: "Hakika Misikiti hii haifai kuwekwa chochote katika mikojo hii, wala uchafu wowote, bali hii ni kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuswali, na kusoma Qur'ani" Au kama alivyosema Mtume rehema na amani ziwe juu yake, anasema; akumuamrisha mtu mmoja miongoni mwao akaja na ndoo ya maji akapamwagia.

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 285]

Ufafanuzi

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake msikitini kwake akiwa pamoja na Maswahaba zake, akaja bedui mmoja kutoka kijijini, akaanza kukojoa katika kona ya msikiti. Maswahaba wakamkaripia na wakasema: Koma, na wacha unachokifanya. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Muacheni, na wala msimkatishe mkojo wake, wakamuacha mpaka akamaliza.
Kisha rehema na amani ziwe juu yake akamuita na akamwambia: Hakika misikiti haifai kwa chochote miongoni mwa mikojo hii, wala aina yoyote ya uchafu, bali ni kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na swala, na kusoma Qur'ani na mfano wa hayo. Kisha akamuamrisha rehema na amani ziwe juu yake mtu mmoja katika Maswahaba akaja na ndoo iliyojaa maji akayamwaga katika mkojo wake.

Katika Faida za Hadithi

  1. Uwajibu wa kuitukuza misikiti, na kuilinda na yale yasiyofaa.
  2. Amesema Nawawi: Hapa kuna kuilinda misikiti na kuitakasa kutokana na uchafu na takataka na mate, na kunyanyua sauti na ugomvi, na kuuuza na kununua, na mikataba yote, na yenye kufanana na hayo.
  3. Kumuhurumia mjinga na kumfundisha yanayompasa bila kumkaripia wala kumuudhi ikiwa hatofanya kosa kwa kudharau au makusudi.
  4. Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni mwalimu mpole, na muadabishaji mwenye huruma, na mlezi mwenye huruma.
  5. Himizo la kuziimarisha nyumba za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa swala na Qur'ani na kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama