عَنْ أَبِي طَلْحَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«لاَ تَدْخُلُ المَلاَئِكَةُ بَيْتًا فِيهِ كَلْبٌ وَلاَ صُورَةٌ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 3322]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Hawaingii Malaika nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha"
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 3322]
Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika wa rehema hawaingii nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha za viumbe hai; Hii ni kwa sababu sura ya kitu ambacho kina roho ni dhambi kubwa, na kuna uigaji wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu, na ni njia katika njia za ushirikina, na baadhi yake ni picha ya vile vinavyoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu. Ama sababu ya kujiepusha na nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa; ni kwa sababu anakula uchafu mwingi, na ni kwa sababu baadhi mbwa huitwa mashetani; Na malaika wako dhidi ya mashetani. Na kwa sababu ya harufu mbaya ya mbwa; Malaika wanachukia harufu mbaya, na kwa sababu ni haramu kuwafuga; Hivyo mwenye kuwafuga akaadhibiwa kwa kunyimwa Malaika kuingia nyumbani kwake, na kuswali humo, na kumuombea msamaha, kumbariki yeye na nyumba yake, na kumzuilia udhia wa Shetani.