عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال: "أكبر الكبائر: الإشراك بالله، والأمن من مَكْرِ الله، والقُنُوطُ من رحمة الله، واليَأْسُ من رَوْحِ الله".
[إسناده صحيح] - [رواه عبد الرزاق]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdillahi bin Masoud Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kutoka kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake yakwamba yeye amesema: "Madhambi makubwa kuliko yote: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kujiaminisha na vitimbi vya Mwenyezi Mungu, na kukata tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu, Na kufa moyo katika huruma za Mwenyezi Mungu".
[upokezi wake ni sahihi] - [Imepokelewa na Abdul Razaaq]
Ametaja Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi hii madhambi ambayo yanazingatiwa kuwa ni katika madhambi makubwa, nayo: ni kuwekewa Mwenyezi Mungu Mtukufu mshirika katika uumbaji wake na kuabudiwa kwake, na ameanza na hili, kwasababu ndiyo dhambi kubwa kuliko yote, na kukata matarajio na matumaini kwa Mwenyezi Mungu; kwasababu huko ni kumdhania vibaya Mwenyezi Mungu na ni kutojua upana wa rehema zake, na kujiaminisha kwa kumvuta taratibu mja kwa kumpa neema ili mpaka aje kumchukua akiwa kaghafilika, na si makusudio ya hadithi kudhibiti idadi ya madhambi makubwa kuwa hakuna zaidi ya haya yaliyotajwa, lakini makusudio yake ni kubainisha makubwa yake.