عَنْ عَلِيٍّ رضي الله عنه:
أَنَّ فَاطِمَةَ رَضيَ اللهُ عنْها أَتَتِ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ تَشْكُو إِلَيْهِ مَا تَلْقَى فِي يَدِهَا مِنَ الرَّحَى، وَبَلَغَهَا أَنَّهُ جَاءَهُ رَقِيقٌ، فَلَمْ تُصَادِفْهُ، فَذَكَرَتْ ذَلِكَ لِعَائِشَةَ، فَلَمَّا جَاءَ أَخْبَرَتْهُ عَائِشَةُ، قَالَ: فَجَاءَنَا وَقَدْ أَخَذْنَا مَضَاجِعَنَا، فَذَهَبْنَا نَقُومُ، فَقَالَ: «عَلَى مَكَانِكُمَا» فَجَاءَ فَقَعَدَ بَيْنِي وَبَيْنَهَا، حَتَّى وَجَدْتُ بَرْدَ قَدَمَيْهِ عَلَى بَطْنِي، فَقَالَ: «أَلاَ أَدُلُّكُمَا عَلَى خَيْرٍ مِمَّا سَأَلْتُمَا؟ إِذَا أَخَذْتُمَا مَضَاجِعَكُمَا -أَوْ أَوَيْتُمَا إِلَى فِرَاشِكُمَا- فَسَبِّحَا ثَلاَثًا وَثَلاَثِينَ، وَاحْمَدَا ثَلاَثًا وَثَلاَثِينَ، وَكَبِّرَا أَرْبَعًا وَثَلاَثِينَ، فَهُوَ خَيْرٌ لَكُمَا مِنْ خَادِمٍ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 5361]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Ally -radhi za Allah ziwe juu yake-:
ِAlikuja Fatma radhi za Allah ziwe juu yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akimlalamikia juu ya jiwe la kusagia lililokuwa likichubua mikono yake, na zilimfikia taarifa kuwa Mtume amejiwa na mjakazi, lakini alikuwa hajakutana naye, akalieleza hilo kwa Aisha, alipokuja Aisha akamwambia, anasema Fatma: Akaja kwetu hali yakuwa tumekwisha panda kitandani, basi tukaamka tukasimama, akasema: "Haina haja ya kusimama kaeni tu mahala penu" Akaja akakaa kati yangu na Fatma, mpaka nikahisi ubaridi wa miguu yake tumboni kwangu, Mtume akasema: «Je, nisikujulisheni kitu bora zaidi kuliko hicho mlichoomba? Mtakapokwenda kulala basi msabihini Mwenyezi Mungu; yaani (Sub-haanallaah) mara thelathini na tatu, na mhimidini (Al-hamdulillaah) mara thelathini na tatu, na mtukuzeni (Allahu Akbar) mara thelathini na nne, kufanya hivyo ni bora zaidi kwenu kuliko mfanyakazi.”
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 5361]
Fatima Mwenyezi Mungu amuwie radhi binti wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alilalamikia athari za mashine ya kusagia (Jiwe) aliyoipata mkononi mwake, hivyo alipokuja mtumwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuendea na kumuomba ampe mmoja kati ya watumwa hao, ili amsaidia kwa kazi za nyumbani, lakini hakumkuta Mtume nyumbani kwake, ila alimkuta Aisha Mwenyezi Mungu amuwie radhi, hivyo akamwambia kuhusu hilo, Alipofika rehema na amani ziwe juu yake Aisha akamueleza kuwa Fatma alikuja kwake kumuomba mfanyakazi. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaja kwa Fatma na Ally Mwenyezi Mungu awawie radhi, ndani ya nyumba yao wakiwa wamelala kitandani wakijiandaa kwa usingizi, akakaa katikati yao mpaka Ally radhi za Allah ziwe juu yake akahisi ubaridi wa miguu ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, juu ya tumbo lake, akasema: Hivi nisikufundisheni kilicho bora zaidi kuliko mlichoniomba, kuliko kukupeni mtumishi? Wakasema: Ndio, tufundishe, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Mtakapochukua nafasi zenu za kulala usiku, basi toeni takbira mara thelathini na nne, kwa kusema: Allahu Akbaru, Na toeni tasbihi mara thelathini na tatu, kwa kusema: Sub-haanallaah, Na himidini mara thelathini na tatu, kwa kusema: Al-hamdulillah; Dhikiri hii ni bora sana kwenu nyinyi kuliko kuwa na mtumishi.