+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عنه سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ:
«قَالَ اللهُ تَعَالَى: قَسَمْتُ الصَّلَاةَ بَيْنِي وَبَيْنَ عَبْدِي نِصْفَيْنِ، وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ، فَإِذَا قَالَ الْعَبْدُ: {الْحَمْدُ لِلهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ}، قَالَ اللهُ تَعَالَى: حَمِدَنِي عَبْدِي، وَإِذَا قَالَ: {الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ}، قَالَ اللهُ تَعَالَى: أَثْنَى عَلَيَّ عَبْدِي، وَإِذَا قَالَ: {مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ}، قَالَ: مَجَّدَنِي عَبْدِي، -وَقَالَ مَرَّةً: فَوَّضَ إِلَيَّ عَبْدِي-، فَإِذَا قَالَ: {إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ}، قَالَ: هَذَا بَيْنِي وَبَيْنَ عَبْدِي وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ، فَإِذَا قَالَ: {اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ، صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلا الضَّالِّينَ}، قَالَ: هَذَا لِعَبْدِي وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 395]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Nimeigawa swala baina yangu na mja wangu nusu mbili, na mja wangu ana haki ya kupata alichooomba, atakaposema mja: "Al-hamdulillaahi rabbil aalamiin" (Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu), Mwenyezi Mungu Mtukufu husema: "Amenihimidi mja wangu", na akisema: "Ar-Rahmaanir Rahiim" (Mwingi wa rehema mwenye kurehemu) Mwenyezi Mungu Mtukufu husema: Kanisifu mja wangu, na akisema: "Maaliki yaumid-diin" (Mmiliki wa siku ya malipo) husema: Kanitukuza mja wangu, na mara nyingine husema: Kakabidhi kwangu mja wangu, akisema: "Iyyaaka na'budu wa iyyaaka nastaiin" (Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada) husema: Hili ni kati yangu mimi na mja wangu, na mja wangu ana haki ya kupata alichokiomba, akisema: "Ihdinas swiraatwal mustaqiim swiraatwalladhiina an amta alaihim, ghairil maghdhuubi alaihim waladh dhwaalliin", husema: Hili ni la mja wangu na mja wangu ana haki ya kupata alichoomba".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 395]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika hadithil Qudsiy: Nimeigawanya suratul fatiha ndani ya swala kati yangu na mja wangu nusu mbili, nusu moja ya kwangu, na nusu moja ya kwake.
Nusu yake ya kwanza: Himdi na sifa na kumtukuza Mwenyezi Mungu, nitamlipa kwa hayo malipo bora zaidi.
Na nusu yake ya pili: Unyenyekevu na dua, ninamuitikia na ninampa alichoomba.
Msaliji akisema: "Al-hamdulillaahi rabbil aalaamiin", Mwenyezi Mungu husema: Amenihimidi mja wangu, na akisema: "Ar-Rahmaanir Rahiim", husema Mwenyezi Mungu: Amenisifu mja wangu akanihimidi na akakiri kutoka kwangu neema zangu zote juu ya viumbe wangu, na akisema: "Maaliki yaumid-diin", husema Mwenyezi Mungu: Amenitukuza mja wangu, nayo ni heshima kubwa.
Akisema: "Iyyaakana'budu wa iyyaaka nastaiin", Mwenyezi Mungu husema: Hili ni kati yangu mimi na mja wangu.
Nusu ya kwanza katika aya hii ni ya Mwenyezi Mungu nayo ni: "Iyyaakana'budu" Nayo ni kukiri uungu kwa Mwenyezi Mungu, na kuitika wito wa ibada, na kwake ndiko inakoishia nusu ambayo ni yake Mwenyezi Mungu.
Na nusu ya pili katika aya nayo ni ya mja: "Iyyaakanastaiinu" Ni kutaka msaada kwa Allah, na kamuahidi kumsaidia.
Akisema: "Ihdinas swiraatwal mustaqiim * Swiraatwalladhiina an amta alaihim, ghairil maghdhuubi alaihim waladh dhwaalliin", Mwenyezi Mungu husema: Huu ni unyenyekevu na ni dua kutoka kwa mja wangu, na mja wangu anastahiki kupata alichoomba, na tayari nimejibu dua yake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Kituruki Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف Luqadda Asariga الأوكرانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Utukufu wa suratul faatiha kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu kaiita kuwa ni swala.
  2. Kumebainishwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kumshughulikia mja wake, kiasi kwamba amemsifia kwa sababu ya kumhimidi na kumsifia kwake na kumtukuza kwake, na akamuahidi kumpa alichoomba.
  3. Sura hii tukufu imekusanya, kumhimidi Mwenyezi Mungu, na kukumbuka marejeo, na kumuomba Mwenyezi Mungu, na kutakasa ibada kwa ajili yake, na kuomba uongofu katika njia iliyo nyooka, na tahadhari ya njia za batili.
  4. Kuvuta hisia za hadithi hii mwenye kuswali -anaposoma suratul fatiha- kutaongeza utulivu wake ndani ya swala.