عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «لَأَنْ أَقُولَ: سبحان الله، والحمد لله، ولا إله إلا الله، والله أكبر، أَحَبُّ إلَيَّ مِمَّا طَلَعَتْ عليْه الشمسُ».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu- Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Kusema kwangu Sub-haana llaah, wal hamdulillaah, wa laa ilaaha illa llaahu wallaahu Akbaru,- Ametakasika Mwenyezi Mungu na kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu na hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu Mkubwa, kunapendeza zaidi kwangu kulikovyote vilivyomo chini ya jua".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Hadithi ndani yake kuna himizo la kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kumtakasa na kumsifu na kumtukuza na kumpwekesha na kumkweza, na nyiradi ni bora kuliko dunia na vilivyomo; kwasababu hii ni katika matendo ya Akhera, nayo ni katika mema yenye kubakia, na thawabu zake hazitoweki, na malipo yake hayakatiki, wakati dunia inaelekea katika kutoweka.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuhimizwa juu kumtaja Mwenyezi Mungu kwa kumtakasa yeye na kumtukuza yeye na kumsifu na kumhimidi yeye na kumkweza.
  2. Sub-haana llaah, wal hamdulillaah, wa laa ilaaha illa llaahu wallaahu Akbaru,- Ametakasika Mwenyezi Mungu na kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu na hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu Mkubwa. Haya ndio mema yenye kubakia.
  3. Starehe za dunia ni ndogo na matamanio yake ni yenye kuondoka.
  4. Neema ya Akhera haiondoki wala haibadiliki.