+ -

عَنِ أبي زُهير عُمَارَةَ بْنِ رُؤَيْبَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم:
«لَنْ يَلِجَ النَّارَ أَحَدٌ صَلَّى قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ غُرُوبِهَا»

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 634]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Zuhairi Umara bin Ruaiba radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Kamwe, hatoingia motoni mtu yeyote aliyeswali kabla ya kuchomoza Jua na kabla ya kuzama kwake"

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 634]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa hatoingia motoni mtu yeyote aliyeswali swala ya Alfajiri, na swala ya Lasiri, na akadumu nazo; na amezitaja maalumu swala hizi mbili; kwa sababu ndizo swala nzito zaidi, na kwa sababu wakati wa Alfajiri huwa ni wakati wa usingizi na ladha yake, na wakati wa Lasiri huwa ni wakati wa kushughulishwa na kazi za mchana na biashara zake, na atakayezihifadhi swala hizi mbili pamoja na kupatikana tabu ndani yake, basi bila shaka ataweza kuzihifadhi swala zingine zilizobakia.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الرومانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Ubora wa swala mbili, Alfajiri na Lasiri, ni lazima kuzihifadhi.
  2. Na atakayezitekeleza swala hizi mara nyingi nafsi yake huepukana na uvivu na kujionyesha na hupenda ibada.