+ -

عَنِ الأَسْوَدِ بنِ يَزِيدَ قَالَ:
سَأَلْتُ عَائِشَةَ مَا كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَصْنَعُ فِي بَيْتِهِ؟ قَالَتْ: كَانَ يَكُونُ فِي مِهْنَةِ أَهْلِهِ -تَعْنِي خِدْمَةَ أَهْلِهِ-، فَإِذَا حَضَرَتِ الصَّلاَةُ خَرَجَ إِلَى الصَّلاَةِ.

[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 676]
المزيــد ...

Kutoka kwa Aswadi bin Yadizi amesema:
Nilimuuliza Aisha, nini alikuwa akifanya Mtume rehema na amani ziwe juu yake nyumbani kwake? Akasema: Alikuwa akishiriki katika kazi za familia yake (anakusudia kuhudumia familia yake), unapofika wakati wa swala anatoka kwenda katika swala.

[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 676]

Ufafanuzi

Aliulizwa mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kuhusu hali ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake nyumbani kwake, na alikuwa akifanya nini? Akasema: Alikuwa ni mtu kama watu wengine, na anafanya wanayofanya wanaume katika majumba yao, anashughulika na kujihudumia yeye na familia yake; anakamua mbuzi wake mwenyewe, na anashona nguo yake, na anashona kiatu chake, na anatengeneza ndoo yake, na ulikuwa unapofikia wakati wa kusimamishwa swala anatoka kwa ajili yakusali rehema na amani ziwe juu yake bila kuchelewa.

Katika Faida za Hadithi

  1. Ukamilifu wa unyenyekevu wake rehema na amani ziwe juu yake na wema wake kwa familia yake.
  2. Amali za kidunia hazitakiwi kumshughulisha mja akawacha swala.
  3. Kuhifadhi kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala, mwanzo wa wakati wake.
  4. Amesema bin Hajari: Na hapa kunahimizo la kuwa mnyenyekevu na kuacha kiburi na mwanaume kuihudumia familia yake.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama