عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلَّى الله عليه وسلم قال:
«ما مِنْ أحَدٍ يُسلِّمُ علي إلا ردَّ اللهُ عليَّ رُوحي حتى أردَّ عليه السَّلامَ».
[إسناده حسن] - [رواه أبو داود وأحمد] - [سنن أبي داود: 2041]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Hakuna yeyote atakayenisalimia isipokuwa Mwenyezi Mungu hunirudishia roho yangu ili nimjibu salam".
[Upokezi wake ni mzuri] - - [سنن أبي داود - 2041]
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hurejeshewa roho yake ili ajibu salam kwa kila aliyemsalimia sawa sawa awe karibu au mbali; na maisha ya Akhera na kaburini ni jambo la ghaibu, hakuna ajuaye uhalisia wake isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee, naye juu ya kila kitu ni muweza.