+ -

عَنْ عُثْمَانَ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«مَا مِنَ امْرِئٍ مُسْلِمٍ تَحْضُرُهُ صَلَاةٌ مَكْتُوبَةٌ فَيُحْسِنُ وُضُوءَهَا وَخُشُوعَهَا وَرُكُوعَهَا، إِلَّا كَانَتْ كَفَّارَةً لِمَا قَبْلَهَا مِنَ الذُّنُوبِ، مَا لَمْ يُؤْتِ كَبِيرَةً، وَذَلِكَ الدَّهْرَ كُلَّهُ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 228]
المزيــد ...

kutoka kwa Othmani Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
"Hakuna Muislamu yeyote atafikiwa na Sala ya lazima kisha akaufanya vizuri udhu wake, na Unyenyekevu wake na Rakaa zake, isipokuwa inakuwa ni kifuta madhambi yaliyo kuwa kabla ya Sala, kwa muda ambao hajafanya madhambi makubwa, na hivyo ndivyo ilivyo kila siku".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 228]

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hakuna muislamu atakayekutwa na wakati wa swala ya faradhi akatawadha vizuri udhu wake na ukaukamilisha, kisha akawa na unyenyekevu ndani ya swala yake kiasi kwamba ukawa moyo wake na viungo vyake vyote vimeelekea kwa Mwenyezi Mungu akivuta picha ya utukufu wake, na akatimiza vitendo vya swala kama rukuu na sijida na vinginevyo, isipokuwa swala hii itakuwa ni kifutio cha madhambi madogo madogo yaliyokuwa kabla yake, madam hajafanya dhambi katika madhambi makubwa, na fadhila hii ni endelevu kwa muda wote na katika kila swala.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Swala inayofuta madhambi ni ile ambayo mja katawadha vizuri udhu wake, na akaitekeleza kwa unyenyekevu akitafuta radhi za Mwenyezi Mungu kwa swala hiyo.
  2. Fadhila za kudumu katika ibada, nakuwa ibada ni sababu ya kusamehewa madhambi madogo.
  3. Fadhila za kutawadha vizuri, na kuswali vizuri pamoja na utulivu ndani yake.
  4. Umuhimu wa kuyaepuka madhambi makubwa ili kusamehewa madhambi madogo.
  5. Madhambi makubwa hayafutwi ila kwa toba.