+ -

عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ لِي رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«أُنْزِلَ -أَوْ أُنْزِلَتْ- عَلَيَّ آيَاتٌ لَمْ يُرَ مِثْلُهُنَّ قَطُّ، الْمُعَوِّذَتَيْنِ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 814]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Uqba bin Aamir -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Zimeteremshwa kwangu aya, hazijawahi kuonekana mfano wake katu, sura mbili za kinga"

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 814]

Ufafanuzi

Ameeleza Ukba bin Aamiri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema kumwambia: Usiku huu Mwenyezi Mungu kaniteremshia aya, hazijawahi kuonekana mfano wake katu -yaani katika kuomba kinga- nazo ni sura mbili za kinga: Suratu (Qul Auudhubirabbil falaq), na suratu (Qul Auudhubirabbin naas).

Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kisin-hala Kivetenamu Kihausa Thai Kiassam الأمهرية الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa ukubwa wa fadhila wa sura mbili hizi.
  2. Himizo la kuomba kinga kupitia sura hizi dhidi ya kila shari.