عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَنْ صَلَّى صَلاَتَنَا وَاسْتَقْبَلَ قِبْلَتَنَا وَأَكَلَ ذَبِيحَتَنَا فَذَلِكَ المُسْلِمُ الَّذِي لَهُ ذِمَّةُ اللَّهِ وَذِمَّةُ رَسُولِهِ، فَلاَ تُخْفِرُوا اللَّهَ فِي ذِمَّتِهِ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 391]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake:
"Atakayeswali swala yetu na akaelekea kibla chetu na akala kichinjwa chetu basi huyo ni Muislamu mwenye dhima ya Mwenyezi Mungu na dhima ya Mtume wake, msimfanyie hiana Mwenyezi Mungu katika dhima yake".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 391]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayeshikamana na nembo za dini za wazi akaswali mfano wa swala yetu, na akaelekea upande wa Ka'aba Kibla yetu, na akala kichinjwa chetu kwa kuamini kuwa ni halali; basi huyu ndio Muislamu ambaye anadhima ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na ahadi yake, msitengue amani ya Mwenyezi Mungu na ahadi yake ndani yake.