عَنْ سَعْدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ:
كُنْتُ أَرَى رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُسَلِّمُ عَنْ يَمِينِهِ، وَعَنْ يَسَارِهِ، حَتَّى أَرَى بَيَاضَ خَدِّهِ.
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 582]
المزيــد ...
Kutoka kwa Sa'd radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Nilikuwa nikimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitoa salamu kuliani kwake, na kushotoni kwake, mpaka ninaona weupe wa shavu lake.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 582]
Ameeleza Sa'di bin Abii Waqasi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba alikuwa akiona shavu la Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokana na kugeuka kwake sana anapotoa salamu kwa ajili ya swala yake, kuliani kwake kwa ajili ya salamu ya kwanza, na kushotoni kwake kwa ajili ya salamu ya pili.