عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ عَنَمَةَ، قَالَ:
رَأَيْتُ عَمَّارَ بْنَ يَاسِرٍ دَخَلَ المَسْجِدَ فَصَلَّى، فَأَخَفَّ الصَّلَاةَ، قَالَ: فَلَمَّا خَرَجَ، قُمْتُ إِلَيْهِ، فَقُلْتُ: يَا أَبَا اليَقْظَانِ، لَقَدْ خَفَّفْتَ، قَالَ: فَهَلْ رَأَيْتَنِي انْتَقَصْتُ مِنْ حُدُودِهَا شَيْئًا؟! قُلْتُ: لَا، قَالَ: فَإِنِّي بَادَرْتُ بِهَا سَهْوَةَ الشَّيْطَانِ، سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: « إِنَّ الْعَبْدَ لَيُصَلِّي الصَّلَاةَ، مَا يُكْتَبُ لَهُ مِنْهَا إِلَّا عُشْرُهَا، تُسْعُهَا، ثُمُنُهَا، سُبُعُهَا، سُدُسُهَا، خُمُسُهَا، رُبُعُهَا، ثُلُثُهَا نِصْفُهَا».
[حسن] - [رواه أحمد] - [مسند أحمد: 18894]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdallah bin Anama, amesema:
Nilimuona Ammari bin Yasiri aliingia Msikitini akaswali, akaifanya swala kuwa fupi, akasema: Alipotoka, Nilisimama kwa ajili ya kumfuata, kisha nikasema: Ewe baba Yakdhani, umefupisha sana, akasema: Je, umeniona nimepunguza chochote katika mipaka yake?! Nikasema: Hapana, akasema: Hakika mimi nilikwenda mbio ili kukwepa kusahaulishwa na Shetani, nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika mja anaweza kuswali swala, hakuna anachoandikiwa isipokuwa moja ya kumi yake, moja ya tisa yake, nane ya kumi yake, saba ya kumi yake, sita ya kumi yake, tano ya kumi yake, robo yake, theluthi yake, nusu yake".
[Ni nzuri] - [Imepokelewa na Ahmad] - [مسند أحمد - 18894]
Aliingia Ammari bin Yasiri radhi za Allah ziwe juu yake Msikitini akaswali swala ya sunna, na ilikuwa swala fupi sana, alipotoka msikitini, Abdallah ibin Anama alimfuata na akasema kumwambia: Ewe baba Yakdhani, nimekuona umefupisha swala yako!. Akasema Ammari: Je, umeniona nimepunguza chochote katika nguzo zake na wajibu wake na sharti zake?! Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Hakika mja anaweza kuswali swala, na asiandikiwe malipo yoyote isipokuwa moja yake ya kumi, au tisa ya kumi, au nane ya kumi, au saba ya kumi, au sudusi yake, au tano ya kumi, au robo yake, au theluthi yake, au nusu yake.