+ -

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مُغَفَّلٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم:
«بَيْنَ كُلِّ أَذَانَيْنِ صَلَاةٌ، بَيْنَ كُلِّ أَذَانَيْنِ صَلَاةٌ» ثُمَّ قَالَ فِي الثَّالِثَةِ: «لِمَنْ شَاءَ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 627]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Amru -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Kati ya kila adhana mbili kuna swala, kati ya kila adhana mbili kuna swala" Kisha akasema katika mara ya tatu: "Kwa atakayetaka"

-

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa baina ya kila adhana na ikama kuna swala ya sunna, na akalirudia hilo mara tatu, na akaeleza katika mara ya tatu kuwa hilo ni sunna na inapendeza kwa atakayetaka kuswali.

Tafsiri: Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Kisin-hala Kivetenamu Kitagalogi Kihausa Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Inapendeza kuswali baina ya adhana na ikama.
  2. Muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kuirudiarudia kauli, na hii ni kwakutaka isikike vizuri na kutia mkazo kwa umuhimu wa yale anayoyasema.
  3. Makusudio ya dhana mbili: Ni adhana na ikama, na zimeitwa zote kuwa ni adhana kama kuichanganya ikama ndani ya adhana, kama kusema miezi miwili (Jua na Mwezi) na akina Omari wawili, yaani: (Abubakari na Omari).
  4. Adhana ni tangazo la kuingia kwa wakati, na ikama ni tangazo la kuwadia muda wa kuswali.