+ -

عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«إِذَا قَالَ الْمُؤَذِّنُ: اللهُ أَكْبَرُ اللهُ أَكْبَرُ، فَقَالَ أَحَدُكُمُ: اللهُ أَكْبَرُ اللهُ أَكْبَرُ، ثُمَّ قَالَ: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، قَالَ: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، ثُمَّ قَالَ: أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ، قَالَ: أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ، ثُمَّ قَالَ: حَيَّ عَلَى الصَّلَاةِ، قَالَ: لَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللهِ، ثُمَّ قَالَ: حَيَّ عَلَى الْفَلَاحِ، قَالَ: لَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللهِ، ثُمَّ قَالَ: اللهُ أَكْبَرُ اللهُ أَكْبَرُ، قَالَ: اللهُ أَكْبَرُ اللهُ أَكْبَرُ، ثُمَّ قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ مِنْ قَلْبِهِ دَخَلَ الْجَنَّةَ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 385]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Omar Bin Khattwab- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-
"Atakapo sema Muadhini: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema mmoja wenu: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema: Ash-hadu An laa ilaha ila llahu, akasema: Ash-hadu An laa ilaha ila llahu. kisha akasema: Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullahi, Akasema: Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullahi, kisha akasema: Hayya ala Swalaah, akasema: Laa Haula wala Quwwata ila Billahi, kisha akasema: Hayya ala lfalaah, akasema: Laa Haula walaa Quwwata ila Billahi, kisha akasema: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, akasema: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema: Laa ilaha ila llahu, akasema: Laa ilaha ila llahu, kutoka ndani ya moyo wake, basi ataingia peponi".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 385]

Ufafanuzi

Adhana ni kuwatangazia watu kuwa muda wa swala umeingia, na maneno ya adhana ni maneno yaliyokusanya itikadi ya imani.
Na katika hadithi hii anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kinachotakiwa kisheria wakati wa kusikia adhana, nako msikiaji asema kama anavyosema muadhini, muadhini akisema: "Allahu Akbaru" Mwenye kusikia naye anasema: "Allahu Akbaru" ataendelea hivyo, isipokuwa katika kauli ya muadhini "Hayya alas swalaa", "Hayya alal falaah, atasema mwenye kusikia: "Laa haulaa wala quwwata illaa billaah".
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakaye rudia rudia nyuma ya muadhini kwa utakasifu kutoka moyoni mwake ataingia peponi.
Na maana ya maneno ya adhana ni: "Allahu Akbaru": Yaani: Yeye mtakasifu ni mtakasifu na ni mtukufu na ni mkubwa kuliko kila kitu.
"Ash-hadu an laa ilaaha illa llaah": Yaani: Hapana muabudiwa wa haki zaidi ya Allah.
"Ash-hadu anna Muhammadan Rasuulu llaah" Yaani: Nina kiri na nina shuhudia kwa ulimi wangu na moyo wangu, yakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alimtuma Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ni wajibu kumtii.
"Hayya alas swalaa", Yaani: Njooni katika swala, na kauli ya mwenye kusikia: "Laa haulaa walaa quwwata illa billaah", Yaani hakuna ujanja wa kuvimaliza vikwazo vya ibada, wala nguvu ya kuzifanya na wala uwezo wa chochote ila ni kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
"Hayya alal falaah", Njooni katika sababu ya kufanikiwa, nako ni kufuzu kwa Pepo na kusalimika na moto.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Kituruki Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية التشيكية Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الأوكرانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Fadhila za kumjibu muadhini kwa mfano wa yale anayosema, isipokuwa katika hayyalaa mbili, atasema: "Laa haulaa walaa quwwata illa billaah".