عن قيس بن عاصم رضي الله عنه قال:
أتيتُ النبيَّ صلى الله عليه وسلم أُريدُ الإسلامَ، فأَمَرَني أن أغتَسِلَ بماءٍ وسِدرٍ.
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي] - [سنن أبي داود: 355]
المزيــد ...
Kutoka kwa Kaisi bin Aswim -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Nilimwendea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nikitaka kuwa muislamu, akaniamrisha nioge kwa maji na mkunazi.
[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 355]
Alikuja Kaisi bin Aswim kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitaka kusilimu, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamuamrisha aoge kwa maji na mti wa mkunazi; kwakuwa majani yake hutumika katika usafi; na kwakuwa yana harufu nzuri.