عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رَضيَ اللهُ عنهُ:
أَنَّ رَجُلًا سَمِعَ رَجُلًا يَقْرَأُ: {قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ} يُرَدِّدُهَا، فَلَمَّا أَصْبَحَ جَاءَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَذَكَرَ ذَلِكَ لَهُ، وَكَأَنَّ الرَّجُلَ يَتَقَالُّهَا، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ إِنَّهَا لَتَعْدِلُ ثُلُثَ القُرْآنِ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 5013]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Saidi Al Khudri -radhi za Allah ziwe juu yake-:
Ya kuwa mwanamume mmoja alimsikia mtu akisoma: "Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee." Huku akiirudiarudia. Ilipofika asubuhi, alimjia Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake, na akamueleza hilo. Na ni kana kwamba mwanamume huyo aliona jambo hilo ni jambo dogo. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake akasema: “Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika, hiyo ni sawa na theluthi moja ya Qur'ani."
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 5013]
Ameeleza Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake kwamba mtu mmoja alimsikia bwana mmoja akisoma suratu: "Qul-huwallaahu Ahad" akiikariri kila usiku na wala hazidishi sura nyingine, palivopambazuka alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamsimulia tukio hilo, ni kana kwamba muulizaji anaiona kuwa ndogo, akatoa kiapo rehema na amani ziwe juu yake kwa maana ya kuonyesha msisitizo, akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake hakika sura hiyo inalingana na theluthi ya Qur'ani.