عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ:
لَمَّا نَزَلَتْ عَلَى رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ {لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَإِنْ تُبْدُوا مَا فِي أَنْفُسِكُمْ أَوْ تُخْفُوهُ يُحَاسِبْكُمْ بِهِ اللهُ فَيَغْفِرُ لِمَنْ يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَنْ يَشَاءُ وَاللهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ} [البقرة: 284]، قَالَ: فَاشْتَدَّ ذَلِكَ عَلَى أَصْحَابِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَتَوْا رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ثُمَّ بَرَكُوا عَلَى الرُّكَبِ، فَقَالُوا: أَيْ رَسُولَ اللهِ، كُلِّفْنَا مِنَ الأَعْمَالِ مَا نُطِيقُ، الصَّلَاةَ وَالصِّيَامَ وَالجِهَادَ وَالصَّدَقَةَ، وَقَدِ اُنْزِلَتْ عَلَيْكَ هَذِهِ الآيَةُ وَلَا نُطِيقُهَا، قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَتُرِيدُونَ أَنْ تَقُولُوا كَمَا قَالَ أَهْلُ الكِتَابَيْنِ مِنْ قَبْلِكُمْ سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا؟ بَلْ قُولُوا: سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ المَصِيرُ»، قَالُوا: سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ المَصِيرُ، فَلَمَّا اقْتَرَأَهَا القَوْمُ، ذَلَّتْ بِهَا أَلْسِنَتُهُمْ، فَأَنْزَلَ اللهُ فِي إِثْرِهَا: {آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْهِ مِنْ رَبِّهِ وَالمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِنْ رُسُلِهِ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ المَصِيرُ} [البقرة: 285]، فَلَمَّا فَعَلُوا ذَلِكَ نَسَخَهَا اللهُ تَعَالَى، فَأَنْزَلَ اللهُ عَزَّ وَجَلَّ: {لَا يُكَلِّفُ اللهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِنْ نَسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا} [البقرة: 286] " قَالَ: «نَعَمْ» {رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِنَا} [البقرة: 286] قَالَ: «نَعَمْ» {رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ} [البقرة: 286] قَالَ: «نَعَمْ» {وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا أَنْتَ مَوْلَانَا فَانْصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الكَافِرِينَ} [البقرة: 286] قَالَ: «نَعَمْ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 125]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Ilipoteremka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ni wa Mwenyezi Mungu ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, na chochote mnachokidhihirisha, kati ya viliomo ndani ya nafsi zenu au mnachokificha, Mwenyezi Mungu anakijua, na atawahesabu nacho. Atamsamehe anayemtaka na atampatiliza anayemtaka. Na Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu" [Al-Baqara: 284], anasema: Likawa gumu sana hilo kwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha wakashuka chini kwa kupiga magoti, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu tumepewa jukumu la matendo tunayoyaweza, kama Swala, Swaumu, na Jihadi, na Sadaka, na imeteremka juu yako aya hii wala hatuiwezi, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Je hivi mnataka kusema kama walivyosema watu wa vitabu viwili kabla yenu, tumesikia na tumeasi? bali semeni: Tumesikia na tumetii tunataraji msamaha toka kwako ewe Mola wetu Mlezi, na marejeo ni kwako", wakasema: Tumesikia na tumetii tunataraji msamaha toka kwako ewe Mola wetu Mlezi, na marejeo ni kwako, walipoisoma kauli hiyo, zikadhalilika ndimi zao, akateremsha Mwenyezi Mungu punde tu baada ya hapo: "Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake, na Waislamu, (pia wameamini hivyo) wote wamemwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na vitabu vyake, na Mitume wake hatutofautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na husema tumesikia na tumetii, tunakuomba msamaha Mola wetu na marejeo ni kwako" [Baqara: 285] walipofanya hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akaifuta, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mwenyezi Mungu hailazimishi nafsi yoyote isipokuwa yaliyo sawa na uweza wake. (Faida ya) yale iliyochuma (nafsi hiyo) ni yake na hasara ya yale iliyochuma ni juu yake. (Husema); Mola wetu usitutese kama tukisahau au tukikosa" [Al-Baqara: 286] Akasema: Ndiyo "Mola wetu na usitubebeshe mzigo kama uliowabebesha wale waliokuwa kabla yetu" Akasema: Ndiyo "Mola wetu usitutwike tusiyoyaweza" [Baqara: 286] Akasema: Ndiyo "na utusamehe na utufutie na uturehemu, Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tusaidie juu ya watu makafiri." [Baqara: 286] Akasema: Ndiyo.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 125]
Alipoteremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake kauli yake: "Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyoko mbinguni na Ardhini" Kwa kuviumba na kuvimiliki, na maamuzi na kuvipangilia, "Na ikiwa mtadhihirisha" na mkaonyesha wazi na mkatangaza "yaliko ndani ya nafsi zenu" na vifua vyenu "au mkayaficha" mkayasitiri na kuyaficha ndani ya nyoyo zenu "atakuhesabuni Mwenyezi Mungu" siku Kiyama. "basi anamsamehe amtakaye" kwa fadhila zake na rehema zake, "na anamuadhibu amtakaye" kwa uadilifu wake, "na Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu ni muweza" hakimshindi chochote. Maswahaba walipolisikia hilo liliwapa uzito sana; kwa sababu ndani yake kuna kuadhibiwa mpaka kwa yale yaliyoko moyoni, miongoni mwa fikira. Wakamjia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha wakashuka chini kwa kupiga magoti, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumepewa majukumu kabla ya hili miongoni mwa amali za mwili yale tuwezayo kuyafanya; mfano kama swala na swaumu na Jihadi na sadaka, lakini imeteremshwa kwako aya hii na wala hilo hatuliwezi. Akasema kuwaambia rehema na amani ziwe juu yake: Hivi mnataka kusema kama walivyosema Mayahudi na Wakristo: "Tumesikia na tumeasi"? bali semeni: "Tumesikia na tumetii, tunataraji msamaha kutoka kwako Mola wetu, na marejeo ni kwako", Maswahaba kuitika amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wakasema: Tumesikia na tumetii, tunataraji msamaha kutoka kwako Mola wetu, na marejeo ni kwako. Walipolizungumza hilo Waislamu kwa ndimi zao, na nyoyo zao zikatii; Mwenyezi Mungu akateremsha sifa njema kwa Mtume na Umma wake kwa kauli yake: "Ameamini Mtume yale yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake na waumini (pia wameamini hivyo)" na zikanyenyekea ndimi zao na nyoyo zao kwa amri ya Mwenyezi Mungu. "Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu na Malaika wake na vitabu vyake na Mitume wake, hatutofautishi yeyote katika Mitume wake". Bali tunawaamini wote "na wakasema tumesikia" kauli yako "na tumetii" amri yako, na tunaomba "maghufira yako Mola wetu" na msamaha wako, "na marejeo ni kwao" na mafikio siku itakaposimama hesabu, walipofanya hivyo, na wakasema walichoamrishwa kusema kama kudhihirisha usikivu na utiifu kwa amri za Mwenyezi Mungu; akaupunguzia Mwenyezi Mungu Umma huu na akaifuta aya hiyo, kwa kauli yake: "Hailazimishi Mwenyezi Mungu Nafsi ila kwa kadiri ya wasaa wake" na uwezo wake na nguvu zake na juhudi zake, "ina" thawabu "za yale iliyoyachuma" na kuyafanya miongoni mwa kheri, "na inabeba" adhabu "za yale iliyoyachuma" kama mzigo wa dhambi, na hamuadhibu Mwenyezi Mungu kwa dhambi la mtu mwingine, wala kwa yale yaliyotiwa wasi wasi na nafsi yake. "Mola wetu, usituadhibu" na ukatutesa "ikiwa tutasahau" tukawa hatukukumbuka, "au tukakosea" tukaiacha haki si kwa makusudi, Mwenyezi Mungu akawajibu kwa hilo akasema: Ndiyo, nimefanya hivyo. "Mola wetu Mlezi usitubebeshe mazito" na mashaka na magumu "kama ulivyowabebesha wale waliokuwa kabla yetu" katika wana wa Waisraeli na wengineo, Mwenyezi Mungu akapokea na akasema: Ndiyo, nimefanya hivyo. "Mola wetu Mlezi na wala usitubebeshe tusiyoyaweza" miongoni mwa majukumu na mabalaa na mambo ambayo hatuwezi kuyabeba, akasema Mwenyezi Mungu: Ndiyo nimefanya hivyo, "na utusamehe" madhambi yetu na utufutie, "na utughufirie" madhambi yetu na uyasitiri, "na uturehemu" kwa rehema zako pana, "wewe ndiye Mole wetu" na bwana yetu; "tunusuru" kwa kusimamisha hoja na ushindi "kwa watu makafiri" katika kupigana nao na kupambana nao, Mwenyezi Mungu akapokea, akasema kuwaambia: Naam, nimefanya hivyo.